WANAWAKE WEUSI WENYE NGUVU YA PESA DUNIANI.


Naamini kuna wanawake ambao wanahisi kwamba hawawezi kufanya kitu, wanachodhani kwamba wamezaliwa kwa ajili ya kuhangaikiwa, hawaamini kwamba kama nao watajituma kwenye kufanya kazi, kupanua mawazo yao kibiashara wataweza kufanikiwa.
Kuna wengine nao wanahisi kwamba hata kama watapambana, bado watabaki palepale kwa kuwa tu kuna watu nyuma wanawavuta. Kama una mawazo hayo, ndugu yangu utakuwa unakosea sana kwani kuna wanawake waliopambana na kupata pesa na sasa hivi ni mabilionea wakubwa duniani.
Leo ninakuletea orodha ya wanawake weusi kama wewe ambao wamepambana sana na mwisho wa siku kuwa mabilionea wakubwa, hawakujidharau, walijua kwamba wanaweza kufanikiwa na hivyo kupambana sana na mwisho wa siku kupewa heshima kila walipokuwa.
                                                1.Isabel dos Santos
Unapowazungumzia wanawake weusi wenye pesa duniani basi bila shaka mwanamke huyu atakuwa mtu wa kwanza kuja kichwani mwako. Ni mtoto wa rais wa Angola, Jose Eduardo dos Santos, ni mwanamke ambaye alianza kuzikusanya pesa tangu kipindi kirefu nyuma, akafungua maduka makubwa, vituo vya televisheni, ana migodi ya dhahabu. Anasema kwamba kila pesa anayoipata huwa anaiingiza kwenye mzunguko kwani ukikaa nayo ni lazima utaifanyia matumizi mengine yasiyokuwa na maana.
Ametoa ajira nyingi nchini Angola lakini pia ameingia ubia na kampuni nyingi za Ureno kama Nova Cimangola inayoshughulika na utengenezaji wa saruji, kampuni ya simu ya Telefonica na kampuni nyingine nyingi nchini humo. Utajiri wake ni dola bilioni 3.3 ambazo ni zaidi ya shilingi trilioni 7.
                                                      2. Oprah Winfrey
Ni mwanamke mweusi Mmarekani mwenye umaarufu mkubwa duniani, anaendesha kipindi chake cha Oprah Winfrey Show. Maisha yake ya nyuma yanasikitisha, hakuzaliwa kwenye familia yenye pesa, alikuwa masikini mkubwa ambaye aliishia kubakwa na kupata mimba utotoni.
Katika kupambana kwake, aliwahi hata kukataliwa katika kituo cha televisheni kwa kuonekana hajui. Ila kwa kuwa alidhamiria kupambana usiku na mchana, mwisho wa siku akafanikiwa kwa kuanzisha kipindi chake nchini Marekani ambacho kimekuwa kikiangalia dunia nzima.
Ingekuwaje kama angekubalia kwamba yeye hajui? Ingekuwaje kama angekata tamaa baada ya kukataliwa? Angefika hapo alipokuwa? Wakati mwingine hutakiwi kukata tamaa hata kama mambo yatakuwa magumu kiasi gani. Sasa hivi ana utajiri wa dola bilioni 3 ambazo ni zaidi ya trilioni 6.
                                              3. Folorunsho Alakija
Ni mwanamke mwenye pesa nyingi kuliko wanawake wote nchini Nigeria. Katika maisha yake ya ujanani, hakuwa na ndoto za kuwa bilionea mkubwa, alipanga kuwa mwanamitindo na ndicho kitu kilichompeleka nchini Uingereza.
Ila huko, akafanikiwa na hivyo kuamua kujiingiza katika biashara mbalimbali. Akawekeza kwa wanamitindo, akawa na kampuni kubwa ya uchapishaji na alipoona amepata pesa zaidi akaingia katika uuzaji wa mafuta na kufungua kampuni yake ya Famfa Oil Limited ambayo ndiyo ulimpa pesa zaidi.
Kwa sasa si mwanamitindo tena, anapambana katika uuzaji wa mafuta nchini Nigeria, biashara ambayo imemfanya kunukia pesa na kuwa mtu mwenye mafanikio makubwa mpaka kufikia utajiri wa dola bilioni 2.1 ambazo ni zaidi ya shilingi trilioni 4.2
                                                       4. Sheila Crump Johnson
Ni Mmarekani mwenye pesa ndefu, ndiye mmiliki wa Kituo cha Televisheni cha BET nchini humo. Kwa kuwa alikuwa na pesa, aliamini kwamba kama angekuwa na vitega uchumi mbalimbali basi angeingiza pesa zaidi.
Leo hii, anamiliki timu za mpira wa kikapu nchini humo, Washington Wizard na Washington Mystics, anamiliki hoteli kubwa ya Blue Ridge Mountains. Ni mwanamke ambaye kichwa chake kinafikiria pesa kila siku, si mwanamke wa kukaa na kusema kwamba wenzake wanafanikiwa lakini yeye hana bahati. Unapoamua kupambana, huwezi kubaki hivyohivyo ulivyo kwani Mungu ataangalia juhudi zako, ataangalia jasho lako na kukufungulia mlango wa mafanikio. Sheila anamiliki utajiri wa dola milioni 710 ambazo ni zaidi ya shilingi trilioni 1.4.

Comments


Popular posts from this blog

DROO YA KLABU BINGWA ULAYA HII HAPA

Nyumba ya Mbunge Kigoma Mjini Zitto Kabwe yaungua moto

Wanawake wasiowaita waume kwa majina yao India

Cristiano Ronaldo kawaonesha watoto wake mapacha leo

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO

Baada ya Kifo cha Mumewe… Zari Akwaa Aibu 5 #Tazama

hali ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu

Emmanuel Mbasha, aweka wazi haya .