MBUNGE wa Nzega Mjini, Hussein Bashe ajitolea kwa wazee

MBUNGE wa Nzega Mjini, Hussein Bashe, ametoa vitambulisho vya matibabu bure kwa wazee 3,284 wa jimbo lake huku akisema amefanya hivyo kwa kuwa wazee hao wamelitumikia Taifa kwa muda mrefu na sasa ni vyema vijana wakawahudumia.
Utoaji wa vitambulisho hivyo ni utekelezaji wa Sera ya Taifa Matibabu ya Bure kwa wazee, ambapo baada ya kupata vitambulisho hivyo, itakuwa rahisi kwao kwenda hospitali na kupatiwa matibabu bila malipo.
Katika uzinduzi wa zoezi hilo, Bashe ametoa vitambulisho 540 na vingine vitaendelea kutolewa katika ofisi ya Mbunge iliyopo Nzega Mjini.
Akizungumza na wazee waliojitokeza kupokea vitambulisho hivyo, Bashe alisema: “Wazee hawa wameitumikia nchi hii kwa muda mrefu, ni jukumu letu sasa kama vijana na Taifa kuhakikisha nasi tunawalipa sehemu ya nguvu kubwa walizotumia kuifikisha Tanzania hapa ilipo leo kwa kuwapatia matibabu bora na kuwaondolea gharama za matibabu ili kuleta unafuu wa maisha.
“Nilichokifanya ni kugharamia fedha zote za vitambulisho ili kuhakikisha kila mzee ndani ya Jimbo la Nzega Mjini anapata kitambulisho cha matibabu ya bure.”
Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Godfrey Ngupula,​ ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye zoezi hilo, alimpongeza Bashe kwa kusimamia shughuli za maendeleo na kuwatumikia wananchi kwa moyo wake wote.

Comments


Popular posts from this blog

DROO YA KLABU BINGWA ULAYA HII HAPA

Nyumba ya Mbunge Kigoma Mjini Zitto Kabwe yaungua moto

Wanawake wasiowaita waume kwa majina yao India

Cristiano Ronaldo kawaonesha watoto wake mapacha leo

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO

Baada ya Kifo cha Mumewe… Zari Akwaa Aibu 5 #Tazama

hali ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu

Emmanuel Mbasha, aweka wazi haya .