Michezo:Ajibu huyo yanga
Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa amemtangaza rasmi mshambuliaji, Ibrahim Ajib Migomba kujiunga na timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili.
“Tuna mtambulisha rasmi kwa wapenzi wa Yanga na wanamichezo kwa ujumla mchezaji, Ibrahim Ajib ambaye kwa hivi sasa amepata kandarasi ya miaka miwili kuichezea klabu ya Yanga”.
“Tumekuwa tukisikia kwenye vyombo vya habari na tumekuwa tukisema tutaendelea kutangaza wachezaji kwa wakati maalumu kama ilivyokuwa leo tumeamua kumtangaza rasmi Ajibu na natumia fursa hii kumpokea” amesema Charles Boniface Mkwasa katibu Mkuu wa klabu ya Yanga.
Uwezo wake mkubwa wa kumiliki mpira na kufunga ndio sababu ya wadau wengi kuamini mshambuliaji huyu wa Yanga anaweza kuwa mmoja wa watakao weza kuisadia klabu hiyo katika mashindano ya kitaifa na kimataifa ambayo wanakabiliwa nayo.
Comments