Kesi ya kuzuia Polisi kufanya uchunguzi, inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jamii Forum, Maxence Melo (40) na Mwanahisa wa mtandao huo, Mike Mushi, imeshindwa kuendelea baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha ombi la kuifanyia marekebisho hati ya mashtaka. Kesi hiyo namba 456 ya mwaka 2016, iliyopo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jana ilipaswa kuendelea na ushahidi wa upande wa mashtaka. Wakili wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi alimweleza Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba anayeisikiliza kesi hiyo kuwa, ilikuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi lakini wanaomba kuifanyia marekebisho hati ya mashtaka chini ya kifungu 234 (1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA). Hata hivyo, Wakili wa utetezi, Jeremiah Mtobesya alipinga maombi hayo ya kutaka kufanyia marekebisho ya hati hiyo, akidai kuwa tayari mahakama imeshasikiliza shahidi mmoja wa upande wa mashtaka. “Tunaomba mahakama isikubali upande wa mashtaka kubadilisha hati ya mashtaka kwa sababu hatujaambiwa i