Posts

Showing posts from November, 2017

Magazeti ya Tanzania leo jumapili ya Nov 05_2017

Image
Magazeti ya leo Nov 05, Kurasa za mbele na nyuma michezo udaku na burudani bila kusahau habari mahususi za hardnews kitaifa na Kimataifa

Tundu lissu atuma salamu ychaguzi wa madiwani

Image
Ujumbe huo kutoka kwa Lissu kwenda kwa wapiga kura umefikishwa na Diwani wa Sombetini Arusha, Ally Bananga ambaye amefika hospitali ya Nairobi nchini Kenya anakopatiwa matibabu mbunge huyo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Bananga ameandika, "Nendeni mkawaambie watu kwenye kata zenye uchaguzi kuipa kura ccm ni kufurahia na kuruhusu mateso yetu yaendelee!!... ." Ujumbe alioutoa Lissu kupitia diwani Bananga Ameongeza kwamba 'Hawa watesi wetu wako katika hatua za mwisho, kama wanajiamini kwa nn wanawawekea mizengwe wagombea wetu ili wao wapite bila kupingwa"

Harmorapa atowa yamoyoni

Image
Kwenye ukurasa wake wa instagram, Harmorapa ameandika ujumbe akisema kwamba hatokuja kukata tamaa juu ya ndoto yake ya kumng'oa 'Wema Sepetu na hatimaye kumuweka ndani kama mke wake. “ Naamini sana katika ndoto kua ipo siku ndoto unayoota itatimia na kuwa kweli, sina cha kusema zaidi ya kumpa hongera Dogo Janja, naamini ushupavu na kutovunjika moyo kumemfanya leo akawa mume wa mwanamke wa ndoto zake, nami sivunji imani naamini Wema Sepetu ipo siku atakua wangu, ugumu alioupata Janjaro umenipa matumaini, kikubwa ni kutulia na ndoto yangu na kulenga ipo siku itatimia... One day you will be mine Wema Sepetu” , ameandika Harmorapa.

wananchi wamshtaki polisi kwakuwanyanyasa

Image
Wakitoa malalamiko hayo kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mh. Christina Mndeme ambaye kwa mara ya kwanza amefanya ziara ya kikazi wilayani Tunduru tangu kuteuliwa kwake Octoba kushika wadhifa huo, baadhi ya wananchi hao wa Tunduru wamesema askari huyo amekuwa akiwanyanyasa kwa kuwabambikiza kesi na wakati mwingine kukamata wananchi wakiwa kwenye shughuli za uzalishaji mali akiwaita wazururaji. Akijibu malalamiko hayo ya wananchi, Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Tunduru, Mrakibu Mwandamizi wa jeshi la Polisi, Mwakasanda amesema ameshaagiza askari Polisi huyo akamatwe popote alipo na kuwekwa ndani kwa uchunguzi zaidi. Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mh, Christina Mndeme amewaonya askari polisi kuacha tabia ya kubambikizia kesi wananchi na badala yake watende haki huku akiwataka wananchi wasiogope kutoa taarifa polisi endapo wanafanyiwa vitendo hivyo ili hatua zaidi zichukuliwe.

Chadema wasema haya kuhusu jimbo la nyalanu

Image
Afisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene, alipoulizwa kuhusu uchaguzi huo, alisema watamtangaza mgombea wake, baada ya Nec kutangaza kuhusu uchaguzi huo. "Tutamtangaza mgombea wetu ambaye tutamsimamisha kwenye uchaguzi huo mdogo na tunaamini tutakayemsimamisha lazima atashinda," alisema Makene. Aidha kwa upande wa Mkurugenzi wa NEC, Ramadhani Kailima baada ya kuulizwa iwapo amekwishapata barua kutoka bungeni  na lini itatangaza uchaguzi mdogo wa jimbo hilo, alifunguka na kudai kuwa muda ukifika watatoa taarifa. Kutangazwa kuwa wazi kwa jimbo hilo, sasa kunatoa fursa kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutangaza mchakato wa kupata mrithi wa Lazaro Nyalandu ambaye alitangaza kujizulu nafasi hiyo na kujitoa uanachama wa CCM mwanzoni mwa wiki. Taarifa iliyotolewa jana ilisema Spika wa Bunge, Job Ndugai, amemwandikia Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage, kumfahamisha kuwa jimbo hilo liko wazi. Taarifa ya Bunge ilisema Spika ameandika barua hiyo kwa mujibu wa

Mourinho azidi kumrushia vijembe Antonio Conte.

Image
Mourinho amesisitiza kuwa na mejeruhi sio sababu ya kupata matokeo mabaya na hii moja kwa moja inaonekana ni ujumbe wa meneja wa Chelsea Antonio Conte. Mourinho amesema kama ingekuwa kulalamikia majeruhi ndio kigezo cha kupoteza mechi basi yeye alipaswa kulalamika kila siku kutokana na idadi ya majeruhi kwenye kikosi chake ambao pia ni wachezaji muhimu kwenye timu akiwemo kiungo Paul Pogba. Kocha huyo raia wa Ureno alimshutumu kocha mwenzake Antonio Conte raia wa Italia kuwa analia sana kuhusu majeruhi wakati kila timu ina wachezaji wa akiba ambao wanaweza kutumika wakati ambao wengine wakiwa majeruhi. Mvutano kati ya makocha hao wawili umeendelea kuimarika hususani wiki hii ambapo timu zao zitakutana jumapili ya kesho kwenye uwanja wa Stamford Bridge ukiwa ni mchezo wa 11 wa EPL msimu huu.