Mourinho azidi kumrushia vijembe Antonio Conte.

Mourinho amesisitiza kuwa na mejeruhi sio sababu ya kupata matokeo mabaya na hii moja kwa moja inaonekana ni ujumbe wa meneja wa Chelsea Antonio Conte.
Mourinho amesema kama ingekuwa kulalamikia majeruhi ndio kigezo cha kupoteza mechi basi yeye alipaswa kulalamika kila siku kutokana na idadi ya majeruhi kwenye kikosi chake ambao pia ni wachezaji muhimu kwenye timu akiwemo kiungo Paul Pogba. Kocha huyo raia wa Ureno alimshutumu kocha mwenzake Antonio Conte raia wa Italia kuwa analia sana kuhusu majeruhi wakati kila timu ina wachezaji wa akiba ambao wanaweza kutumika wakati ambao wengine wakiwa majeruhi.
Mvutano kati ya makocha hao wawili umeendelea kuimarika hususani wiki hii ambapo timu zao zitakutana jumapili ya kesho kwenye uwanja wa Stamford Bridge ukiwa ni mchezo wa 11 wa EPL msimu huu.

Comments


Popular posts from this blog

sharti la polepole lapata upinzani

wananchi wamshtaki polisi kwakuwanyanyasa

KENYA:Tume Huru ya Uchaguzi yaridhia maombi ya upinzani

Angelina Jolie kuonekana kwenye jarida la ‘Vanity Fair’.

Afisa wa serikali ajinyonga

Viongozi wa G7 waangazia bara la Afrika

UEFA kuendelea kutimuavumbi hii leo

YANGA YASHUSHA STRAIKA WA AFCON

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO