HUENDA Yanga wakatimiza ahadi yao ya kutangaza ubingwa mapema msimu ujao, hii ni kutokana na usajili wa nguvu wanaoufanya, kwani baada ya kunasa saini ya baadhi ya wachezaji muhimu, sasa wameelekeza nguvu zao nchini Ivory Coast na muda wowote watashusha mtambo wa mabao. Straika huyo, ambaye wanamuwinda kwa udi na uvumba, ni Aristide Bance, ambaye amekipiga katika timu mbalimbali barani Ulaya, ikiwamo Ujerumani pamoja na Afrika. Kwa sasa straika huyo anaichezea timu ya Asec Mimosas ya nchini kwao Ivory Coast, lakini ameshawahi kupita nchini Uturuki akiichezea Samsunspor, pia 1. FSV Mainz 05 ya nchini Ujerumani. Straika huyo ambaye kucheka na nyavu ni jambo la kawaida kwake, pia aliichezea Chipa ya nchini Afrika Kusini katika msimu wa 2015/16, akiifungia jumla ya mabao matatu katika michezo 14 aliyocheza. Kwa ujumla straika huyo mpaka sasa amepitia timu 19, lakini mafanikio yake makubwa aliyapata kwenye soka la Ujerumani pamoja na Ubelgiji, ambapo timu alizozichezea alifunga idadi...
Comments