Posts

Showing posts from May, 2017

HAKIMU AJITOA KESI YA MBUNGE GODBLESS LEMA.

Image
Hakimu mmoja anayesikiliza kesi za Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Godbless Lema amejitoa katika kusikiliza kesi ya kiongozi huyo ambapo baadhi zinatarajiwa kuanza kuunguruma Juni 20 mwaka huu baada ya upelelezi kukamilika. Hakimu amesema kuwa, kiongozi huyo ana jumla ya mshataka manne ya uchochezi ambayo yote yapo mikononi mwake, ndio sababu ameamua kujitoa kusikiliza moja ya mashtaka hayo. Hayo yalisemwa na Hakimu Mkazi Desderi Kamugisha wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ambapo alifafanua amefikio uamuzi huo baada ya kuona si busara kesi zote hizo kuwa mikononi mwake. Hakimu Kamugisha amejitoa katika kesi ya jinai namba 441/2016 ambayo Lema anadaiwa kutoa matamshi ya kumkashifu Rais Dkt Magufuli Oktoba 23, mwaka jana wakati wa mkutano wa hadhara viwanja vya Shule ya Sekondari Baraa. “Kiburi cha Rais akiendelea kujiona yeye ni Mungu, hatafika 2020, Mungu atakuwa amechukua maisha yake. Rais ni mbabe na watu anawaonea, wafanyakazi wa serikali hawana amani, wafanyab

ALICHOSEMA RAIS MAGUFULI BAADA YA KUPOKEA TAARIFA ZA KIFO CHA NDESAMBURO SIASA -

Image
“Kwa masikitiko nimepokea taarifa za kifo cha Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Moshi Mjini, Mzee wangu Philemon Ndesamburo kilichotokea leo tarehe 31 Mei, 2017 katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC iliyopo Moshi Mkoani Kilimanjaro, Namkumbuka Mzee Ndesamburo kwa hekima zake na uongozi wake uliozingatia siasa za kistaarabu” Hii ni kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa katika salamu zake za rambirambi kwa familia ya Marehemu Philemon Ndesamburo, Viongozi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA ) pamoja na ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na kifo hicho. Mhe. Rais Magufuli amesema alifanya kazi na Marehemu Philemon Ndesamburo wakati wote wakiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wakati wote walishirikiana, kutaniana na anamkumbuka kwa namna ambavyo alitumia muda wake bungeni kupigania mambo yenye maslai kwa wananchi wa jimbo lake la Moshi Mjini. Mhe. Dkt. Magufuli ameitaka familia ya Marehemu Phi

Zitto aandika mazito kuhusu kifo cha Ndesamburo

Image
Dar es Salaam. Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo) Zitto Kabwe ametuma salamu za rambi rambi kwa wanachama wa Chadema baada ya kuondokewa na kiongozi wake mkubwa, Philemon Ndesamburo.  Pia Zitto amempa pole, mtoto wa marehemu Ndesamburo, Lucy Owenga kwa kumpoteza baba yake. Zitto ameandika katika ukurasa wake wa Facebook leo na kusema; “Ni msiba mkubwa kwa watu wa Kilimanjaro na hasa Moshi Mjini ambapo Mzee Ndesa Pesa alikuwa mwakilishi wake Bungeni kuanzia Mwaka 2000 mpaka Mwaka 2015. Kilimanjaro imepoteza mtu ambaye aliweka maslahi ya mkoa wake mbele kuliko kitu kingine chochote.” Zitto amesema msiba wa Ndesamburo ni mkubwa kwa wanaChadema ambacho alikuwa Mwenyekiti wake wa Mkoa tangu chama kimeanzishwa mpaka mauti yalipomkuta.  “Huwezi kutaja maendeleo ya Chadema kwa nchi yetu bila ya kutaja jina la mzee Ndesamburo. Nimepata bahati ya kufanya naye kazi kwa karibu, naweza kutamka bila wasiwasi kwamba ni mmoja wa watu waliokipenda chama chake kwa dhati kabisa,” amesema

Video: Liisu awa mbogo tena bungeni kuhusu mchanga wa dhahabu

Image

TANZIA: Aliyewahi kuwa mbunge wa Moshi Mjini, Mzee Philemon Ndesamburo(CHADEMA) aaga dunia

Image
TANZIA: Aliyewahi kuwa mbunge wa Moshi Mjini, Mzee Philemon Ndesamburo(CHADEMA) aaga dunia Taarifa ambazo tumezipata za uhakika muda huu kutoka Mkoani Kilimanjaro aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Moshi Mhe Ndesamburo amefariki muda mfupi uliopita. Taarifa zaidi zitatolewa muda mfupi ujao. ========UPDATES Kwa masikitiko tunawatangazia kuwa, Mbunge Mstaafu wa Moshi Mjini na Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa kilimanjaro, Mhe.Pilemon Ndessamburo amefariki Dunia mapema hii leo. Katibu wa kanda ya Kaskazini Amani Golugwa ====== Mzee Philemon Kiwelu Ndesamburo alizaliwa February 19, 1935. Alikuwa mwanasiasa kupitia chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) pia kufadhili mambo mengi kupitia chama hicho. Mwaka 2000 alifanikiwa kuchaguliwa na wananchi wa Moshi mjini kuwa mbunge wao mpaka mwaka 2015 alipoamua kwa ridhaa yake kutogombea tena jimbo hilo.

IGP Sirro atangaza bingo la milioni 10 Rufiji

Image
Dar es Salaam. Mkuu mpya wa majeshi, IGP Simon Sirro amefanya mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari leo, na kutangaza dau nono la Sh10 milioni kwa atakayetoa taarifa kuhusu mauaji ya Kibiti, Rufiji na Mkuranga. “Niwaambie ukweli kuwa katika hili, maneno yatakuwa machache lakini vitendo vitakuwa vingi zaidi,” amesema katika mkutano huo. Pia IGP Sirro amewatangazia kiama madereva wa bodaboda na kuwataka kuacha kuvunja sheria za barabarani kwa makusudi. “Huu ni wakati wa kutii utawala wa sheria bila shuruti na nimeshaongea na makamanda wa polisi nchi nzima,” amesema BRIEFING  Oktoba 2016 Kadhalika, Oktoba mwaka jana aliyekuwa Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho Ally Milandu aliuawa baada ya kuvamiwa na watu wanne, waliompiga risasi mbili. Novemba, 2016 Novemba mwaka jana, wenyeviti wawili wa vitongoji wa kijiji hicho waliuawa kwa kupigwa risasi. Januari 2017 Januari mwaka huu, katika kijiji cha Nyambunda, kitongoji cha Mkwandara, watu wasiofahamika walimuua mfanyabiash

Manchester United ndio klabu yenye thamani kubwa Ulaya

Image
Manchester United ndio klabu yenye thamani kubwa barani Ulaya ikiwa na thamani ya Yuro bilioni 3 kulingana na kampuni ya biashara ya KPMG. Mabingwa hao wa kombe la Yuropa wanaongoza katika orodha ya thamani ya Kampuni ya KPMG, ikiwa mbele ya mabingwa wa Uhispania Real Madrid na Barcelona. Utafiti huo uliangazia haki za kupeperusha matangazo, faida, umaarufu, uwezo kimchezo na umiliki wa uwanja. Katika utafiti huo uliofanyiwa timu 32, vilabu vya Uingereza vilitawala orodha hiyo vikijaza nafasi sita kati ya 10 bora. Manchester United wampoteza Pogba Rooney: Nitasalia Manchester United Mourinho: Rooney anaweza kuondoka Man Utd Andrea Sartori ambaye ni mkurugenzi wa maswala ya michezo katika kampuni ya KPMG amesema kuwa kwa jumla thamani ya soka imekuwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. ''Huku hilo likielezewa kufuatia kuimarika kwa matangazo, operesheni za biashara za kimataifa, uwekezaji wa vifaa vya umiliki wa kibinafsi, vifaa vya kisasa pamoja na usimamizi mzu

Dk Mwakyembe amlilia anayedaiwa kuchora nembo        

Image
 Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya msanii mkongwe katika fani ya uchoraji Mzee Francis Maige Kanyasu (86), aliyefariki usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Habari, imeeleza kuwa Waziri Mwakyembe amemwelekeza Mtendaji Mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa, Godfrey Mngereza, kushirikiana kwa karibu na ndugu na jamaa wa marehemu katika mazishi yake. “Wizara itahakikisha michango ya wasanii wakongwe kama Mzee Kanyasu, inafuatiliwa kwa karibu na kuwekewa kumbukumbu kwa faida ya vizazi vijavyo.” imesema taarifa hiyo

Kurasa za mbele za magazeti mbalimbali leo Jumatano, May 31. 2017

Image

MASHABIKI WAKERWA NA POST ZA DIAMOND KWENYE MSIBA WA IVAN SSEMWANGA

Image
Baadhi ya Mashabiki wa Zari The Boss Lady waonyeshwa kukerwa na kitendo cha mpenzi wake Zari, Diamond Platnumz kupost picha mbalimbali za Media Tour na akiwa stejini nchini Kenya wakati waubavu wake Zari akiwa kwenye kipindi Kigumu cha Msiba Wa Mzazi mwenzake aliyefariki wiki iliyopita Nchini Afrika Kusuni. “Rafiki mzuri ni yule anayekupa ushauri mzuri ,,, stop to post these images on media in one month period or more, maana umezifungulia kana kwamba unafurahia badala ya kuomboleza ” pole_zari_ze_boss_lady_ alichangia maneno haya katika moja ya picha ambazo ziliwekwa na Zari Kitika Ukurasa wake wa Instragram Tazama Picha post sita za juu zilizo kwenye ukurasa wa instagram wa Diamond Platnumz

Tiger Woods: Sikuwa nimelewa kwa kunywa pombe .

Image
Mchezaji gofu maarufu duniani Tiger Woods amesema hakuwa amekunywa pombe alipokamatwa akiendesha gari jimbo la Florida mapema Jumatatu. Mchezaji huyo alifunguliwa mashtaka ya kuendesha gari akiwa amelewa, lakini amesema ulevi wake ulitokana na dawa alizokuwa amezinywa kwa ushauri wa daktari. "Nafahamu uzito wa kitendo nilichokifanya na nawajibikia kikamilifu vitendo vyangu," amesema. Polisi walitoa picha ya Bw Woods, akionekana kutokuwa nadhifu, nywele zake zikiwa hazijachanwa na macho akiwa ameyatoa nje na kuonekana mwenye uchovu. Alikamatwa katika mji wa Jupiter. "Nataka umma ufahamu kwamba pombe haikuhusika kwa vyovyote vile. Kilichotokea ni madhara ambayo hayakutarajiwa ya kutumia dawa kwa ushauri wa daktari," alisema. "Sikugundua kwamba kuchanganya dawa kungeniathiri sana hivyo." Aliongeza: "Ningependa kuomba radhi kwa dhati familia yangu, marafiki na mashabiki. Nilitarajia nifanye vyema kuliko nilivyofanya." Skabadhi za polisi z

Wanasayansi nchini Marekani wamefanikiwa kupambana na maradhi sugu

Image
Wanasayansi nchini Marekani wamefanikiwa kupambana na maradhi yaliyokuwa sugu kwa dawa za kupambana na vijidudu yaani antibiotics tatizo ambalo lilikuwa tishio dhidi ya sekta ya afya duniani. Watafiti wameiboresha dawa ya sasa, Vancomycin kwa kutengeneza aina nyingine ya dawa. Vancomycin ilikuwa ikipoteza uwezo wake wa kupambana na bacteria aitwae enterococci ambaye husabisha madhara kwenye njia ya haja ndogo na vidonda. Aina mpya ya dawa hii ina nguvu mara elfu moja zaidi na hushambulia vijidudu kwa njia tatu tofauti, kiasi cha vijidudu kushindwa kupambana na dawa hiyo. Inakadiriwa kuwa vijidudu vilivyokuwa vikipambana na dawa za antibiotics husababisha vifo takriban elfu hamsini kila mwaka nchini Marekani na barani Ulaya.

Wanawake wazidi kuikimbia Sudan kusini

Image
Maelfu ya wanawake na watoto kutoka Sudan kusini wamevuka mpaka kuingia nchini Sudan tangu kuanza kwa mwaka huu, wakikimbia ghasia na kitisho cha njaa. Kwa mujibu wa Shirika la Kuwahudumia Wakimbizi Duniani -UNHCR- Karibu Wasudan kusini laki moja na 37 elfu wameingia nchini Sudan tangu Januari mosi, huku wengine zaidi ya laki moja na 31 elfu wakiwa tayari wamewasili nchini humo tangu mwaka 2016. Wafanyakazi wa misaada wanaarifu kuwa wengi ya watu hao wanaowasili sasa ni wanawake na watoto. Mkurugenzi wa Shirika la Msalaba mwekundu, kanda ya Afrika Dokta Faroumata Nafo-Traore wengi wanakuwa wamedhoofika kiafya na wamekuwa na msongo wa mawazo kutokana na hali iliyowatokea huko wanakotoka. Tangu Desemba mwaka 2013 jumla ya wakimbizi laki nne na 17 elfu wa Sudan Kusini waliingia nchini Sudan. Wengi wao wako katika kambi zilizokuwa Mashariki na Kusini mwa Darfur na magharibi na kusini mwa KordofanxKordofanx Habari na BBC

Ndoa haijanipoteza - Amini

Image
Amini amebainisha hayo baada ya maswali mengi ya mashabiki zake kutaka kujua ni jambo gani ambalo limemsibu mpaka kupotea katika 'game' ya muziki kwa kipindi kirefu. "Kuwa kimya kwangu siyo kwa sababu ya kuoa ila mimi napenda kuandaa vitu vizuri vingi ili ninavyoanza kutoa nyimbo inakuwa 'non stop. Sikuwa na nia ya kusuka albamu, nilikuwa naandaa 'single' kwa ajili ya kwenda kutikisa ulimwengu" -alisema Amini. Pamoja na hayo, Amini amesema mpaka sasa ameshamaliza kutengeneza ngoma kumi ambazo anategemea kuzidondosha wakati wowote kutoka sasa.a haijanipoteza - Amini Amini Amini amebainisha hayo baada ya maswali mengi ya mashabiki zake kutaka kujua ni jambo gani ambalo limemsibu mpaka kupotea katika 'game' ya muziki kwa kipindi kirefu. "Kuwa kimya kwangu siyo kwa sababu ya kuoa ila mimi napenda kuandaa vitu vizuri vingi ili ninavyoanza kutoa nyimbo inakuwa 'non stop. Sikuwa na nia ya kusuka albamu, nilikuwa naandaa 'single'

Walimu wa sanaa hawataajiriwa : Kairuki Waziri Angela Kairuki

Image
Walimu wa sanaa hawataajiriwa : Kairuki Waziri Angela Kairuki Angela Kairuki amesema hayo leo bungeni na kudai kila shule itaweza kupata walimu wa sanaa kulingana na mahitaji yao "Utafiti uliofanywa na Ofisi ya Rais Tamisemi mwaka 2015/2016 umebaini kuwepo kwa ziada ya walimu wa masomo ya sanaa wapatao 7463 katika shule za sekondari, kutokana na hali hii serikali inaendelea na zoezi la kuwagawanya walimu hao au kuwa 'redeploy' kwa kuzingatia uwiano na mahitaji halisi ya walimu wa sanaa kwa kila mamlaka za serikali za mitaa ili kila shule iweze kupata walimu wa masomo ya sanaa badala ya kuajiri walimu wapya" -alisema Angela Kairuki Mbali na hilo Waziri Kairuki amesema serikali inaendelea kuajiri watumishi wa kada mbalimbali ambapo katika mwaka wa fedha 2016/2017 watumishi zaidi ya elfu tisa wameajiriwa serikalini. "Katika mwaka wa fedha 2016/17 jumla ya watumishi wa Umma 90721 wamekwisha ajiriwa kwa kuzingatia vipaumbele na mahitaji ya kila mwajiri na kati

RC atangaza kiama wanaoipaka Serikali tope

Image
Makalla ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na wafanyabiashara na wamiliki wa wa hoteli walipokutana kwenye uzinduzi wa hoteli ya kisasa ya Mgwasi Inn iliyopo Mama John Jijini Mbeya. RC atangaza kiama wanaoipaka Serikali tope By Godfrey Kahango, Mwananchi Mbeya. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amewatangazia kiama watu watakaobainika kuipaka tope na kutaka kuichonganisha Serikali na wafanyabiashara kwa kuwakadiria na kuwatoza kiwango cha kodi ambayo ni kinyume na matakwa halisi. Makalla ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na wafanyabiashara na wamiliki wa wa hoteli walipokutana kwenye uzinduzi wa hoteli ya kisasa ya Mgwasi Inn iliyopo Mama John Jijini Mbeya. Amesema kuna watu hususani watumishi wasiokuwa wamaaminifu wamekuwa wakiipaka tope Serikali kwa wafanyabiashara na kuleta chuki na kuiona sio rafiki kwa mfanyabiashara kutokana na kuwakadiria kodi isiyoendana na uhalisia wa biashara yenyewe huku akisisitiza kodi ilipwe kwa kiwango halali na si vinginevyo. “Jam

TANZIA:Mzee anayedaiwa kuchora nembo ya taifa afariki Muhimbili Francis Maige (Ngosha) amefariki

Image
Mzee anayedaiwa kuchora nembo ya taifa afariki Muhimbili Francis Maige (Ngosha) amefariki Francis Maige (Ngosha) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo. Dar es Salaam. Msanii anayedaiwa kuchora nembo ya Adam na Hawa, iliyotumika kitaifa, Francis Maige (Ngosha) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo. Ngosha aliyepelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wiki iliyopita kwa ajili ya matibabu, amefariki dunia saa 2 usiku Mei 29. Taarifa iliyotolewa na uongozi wa Hospitali ya Muhimbili imeeleza kuwa hali ya Ngosha ilibadilika ghafla akiwa hospitali hapo. “Mwili wake umehifadhiwa katika chumba cha maiti hapa Muhimbili na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa na mamlaka husika.” imesema t

Hawa hapa huwenda waka chukuwa nafasi ya Profesa Sospeter Muhongo

Image
Dodoma. Rais John Magufuli, anatarajiwa kufanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri wakati wowote kuanzia sasa ili kujaza nafasi ya waziri wa Nishati na Madini. Nafasi hiyo iliachwa wazi baada ya Profesa Sospeter Muhongo kung’olewa katika wadhifa huo Mei 24, kutokana na ripoti ya kamati maalumu iliyoundwa na Rais, kuchunguza mchanga wa dhahabu katika makontena 277. Kamati hiyo iliyoongozwa na Profesa Abdulkarim Mruma ilisema Kampuni ya Acacia, haikutangaza kiasi cha madini yote yaliyokuwa katika makontena 277 ambayo yalizuiwa kusafirishwa nje kwa amri ya Rais. Matokeo ya kamati hiyo yanaonyesha kuwa thamani ya madini yote yaliyopo kwenye makontena 277 ni kati ya Sh829.4 bilioni na Sh1.439 trilioni, tofauti na thamani iliyotolewa na Acacia ya Sh97.5 bilioni. Hii ni mara ya pili kwa Profesa Muhongo kung’olewa katika wizara hiyo. Januari 24, 2015 alijiuzulu wadhifa huo baada ya kuhusishwa na kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow ikiwa ni shinikizo la Bunge, baada ya kutolewa kwa

Maajabu ya mapacha walioungana

Image
Hawakuweza kujulikana mapema hadi walipofikia umri wa kwenda shule. Hapo ndipo vyombo vya habari vilipotangaza kwa nguvu habari ya watoto wao, baada ya Mwananchi kuiibua.           Miaka 21 iliyopita, familia ya Alfred Mwakikuti na Naomi Mshumbusi ilijaaliwa kupata watoto pacha, Maria na Consolata. Lakini hawakuwa pacha wa kawaida; walikuwa wameungana na hakukuwapo na uwezekano wa kuwatenganisha. Hawakuweza kujulikana mapema hadi walipofikia umri wa kwenda shule. Hapo ndipo vyombo vya habari vilipotangaza kwa nguvu habari ya watoto wao, baada ya Mwananchi kuiibua. Mwaka 2010 walimaliza elimu ya msingi na 2014 elimu ya sekondari na mwaka huu wamemaliza elimu ya juu ya sekondari. Wakati wote huo gazeti hili limekuwa nao pamoja katika kila hatua na sasa linakuletea habari mfululizo za maisha yao kuanzia leo. Mwandishi wetu, Tumaini Msowoya anaongea nao kwa kirefu kuhusu maisha yao, changamoto, mafanikio na matamanio yao. Sasa endelea Kilolo. Acheni Mungu aitwe
Image
Rapa Eminem ameamua kuchukua hatua kwa vitendo kufuatia shambulizi la kigaidi lililochukua uhai wa watu 22 katika tamasha la muziki la Ariana Grande jijini Manchester nchini Uingereza, kwa kuchangisha fedha kuwafuta machozi familia zilizowapoteza wapendwa wao. Rapa huyo ametumia mtandao wake wa Twitter wenye wafuasi zaidi ya milioni 20 kuwahamasisha watu kuchangia fedha ili kufanikisha lengo lake. “Tafadhali niunge mkono katika kuwasaidia waathirika wa Manchester na familia zao, kwa kuchangia kupitia @BritishRedCross na @MENnewsdesk,” alitweet. Eminem pia aliwaelekeza wafuasi wake kwenye ukurasa wa ‘JustGiving’ ambao alijiunga nao hivi karibuni kwa lengo la kuchangia waathirika, alipotoa tangazo kuwa atarudi jijini Manchester kufanya tamasha lenye faida kwa waathirika. Hadi sasa ukurasa huo umeshachangisha zaidi ya $2.2 million. Katika hatua nyingine, Eminem amewaonjesha mashabiki wake mpango wa kuwapa kitu kipya kwenye tamasha lake la kumbukumbu ya miaka 15 ya albam yake y

Msanii wa Marekani Rapa Eminemana ajipanga kuwafuta machozi waathirika ugaidi Manchester

Image
Rapa Eminem ameamua kuchukua hatua kwa vitendo kufuatia shambulizi la kigaidi lililochukua uhai wa watu 22 katika tamasha la muziki la Ariana Grande jijini Manchester nchini Uingereza, kwa kuchangisha fedha kuwafuta machozi familia zilizowapoteza wapendwa wao. Rapa huyo ametumia mtandao wake wa Twitter wenye wafuasi zaidi ya milioni 20 kuwahamasisha watu kuchangia fedha ili kufanikisha lengo lake. “Tafadhali niunge mkono katika kuwasaidia waathirika wa Manchester na familia zao, kwa kuchangia kupitia @BritishRedCross na @MENnewsdesk,” alitweet. Eminem pia aliwaelekeza wafuasi wake kwenye ukurasa wa ‘JustGiving’ ambao alijiunga nao hivi karibuni kwa lengo la kuchangia waathirika, alipotoa tangazo kuwa atarudi jijini Manchester kufanya tamasha lenye faida kwa waathirika. Hadi sasa ukurasa huo umeshachangisha zaidi ya $2.2 million. Katika hatua nyingine, Eminem amewaonjesha mashabiki wake mpango wa kuwapa kitu kipya kwenye tamasha lake la kumbukumbu ya miaka 15 ya albam yake ya tat

W.C.B MARUFUKU NIGHT CLUB

Image
Kama wewe ni mtembeleaji mzuri wa kurasa za mitandao ya kijamii ya wasanii wa lebo ya WCB inayomilikiwa na Diamond Platinumz, bila shaka umekutana na uhaba mzito wa picha zinazowaonesha wakiwa klabu za usiku. Hii imetokana na marufuku inayowakabili! Mpishi rasmi wa muziki wa WCB ndani ya Wasafi Records, mtarishaji Laizer amesema kuwa moja kati ya sera za lebo hiyo, zinakataza wasanii pamoja na mtayarishaji huyo kwenda kwenye klabu za usiku kula bata. “Moja kati ya vitu ambavyo tunakatazwa ni kwenda klabu za usiku, hii hairuhusiwi kabisa,” Laizer aliiambia Twenzetu ya Times Fm. “Nadhani ni kwa sababu ya brand, haitakuwa kitu kizuri kuona brand inazurula tu usiku kwenye klabu na kama unavyojua klabu za usiku zina mambo mengi,” aliongeza. Hata hivyo alisema kuwa wasanii hao wanaruhusiwa kuingia klabu kama kuna kazi au kuna mwaliko maalum utakaowasilishwa kwenye menejimenti kama mwaliko rasmi. Endelea kubang tu na ngoma za WCB kwenye klabu ya usiku unayoikubali zaidi, lakini usiteg

waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu nchemba awajia juu Chenge, Werema

Image
Wanasheria hao wakuu wa serikali wastaafu, ni Andrew Chenge na Jaji Frederick Werema na amewataka wamwache Rais John Magufuli aendelee kulinda rasilimali za umma, zisiliwe na watu wachache           Iramba.Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amewachana wanasheria wakuu wa Serikali wastaafu kwa kuwataka waeleze hadharani maslahi walionayo kwenye kampuni za madini zinazosafirisha mchanga nje ya nchi. Wanasheria hao wakuu wa serikali wastaafu, ni Andrew Chenge na Jaji Frederick Werema na amewataka wamwache Rais John Magufuli aendelee kulinda rasilimali za umma, zisiliwe na watu wachache. Mwingulu amesema hayo juzi wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na mamia ya wananchi wa Tarafa ya Ndago, jimbo la Iramba. Alisema Chenge na Werema kwa nyakati tofauti wakiwa wanasheria wakuu wa Serikali, pamoja na majukumu yao mengine, wameshiriki kusaini mikataba mikubwa mikubwa, ikiwemo ya makampuni ya kuchimba madini. “Kwa akili ya kawaida tu, baadhi ya mikataba mikubw

IGP Sirro atuma salamu kwa wahalifu nchini

Image
Mkuu wa Jeshi la Polisi, (IGP) Simon Sirro baada ya kuapishwa leo na Rais Magufuli amefunguka na kusema kazi yake ya kwanza kufanya ni kuhakikisha uhalifu unakwisha ili Watanzania waishi kwa amani nchini mwao.     ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mkuu wa Jeshi la Polisi, Kamishna wa Polisi Simon Sirro kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la polisi nchini Mei 29,2017 Ikulu jijini Dar es salaam Simon Sirro amedai uhalifu nchini unaweza kupungua kama kutakuwa na ushirikiano mzuri kati ya wananchi na jeshi la polisi nchini sababu wahalifu hao wanaishi katika jamii zetu hizi hizi. "Kipaumbele kikubwa ni uhalifu hivyo kazi yangu ni kuhakikisha uhalifu unapungua kwa kiasi kikubwa ili Watanzania waishi kwa amani lakini uhalifu huu utapungua tukipata ushirikiano mzuri na jamii, sababu hao wahalifu wanaishi kwenye jamii kwa hiyo ombi langu kwa Watanzania ili waishi kwa amani na utulivu ni vizuri sana watoe ushirikiano kwa jeshi la polisi. Naamin

Kurasa za mbele za magazeti mbalimbali leo Jumatatu May 29

Image