Posts

Showing posts from March, 2018

Magazeti ya Tanzania leo March 24 2018

Image
Pata habari kubwa kwenye Magazeti ya Tanzania March 24 2018 kuanzia ya, Udaku, Michezo na Hardnews kujionea yote makubwa yaliyoandikwa

Jeshi la Polisi Mkoani Tabora lafanya msako

Jeshi la Polisi Mkoani Tabora linawashikilia watu 14 kwa tuhuma za mauaji, wizi pamoja na kukutwa na noti bandia ambazo wamekuwa wakizitumia. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Wilbroad Mutafungwa amesema kuwa watuhumiwa 10 kati ya hao wanaoshikiliwa wanatuhumiwa kwa kosa la mauaji, watatu kwa tuhuma za wizi na mmoja kwa tuhuma za kukutwa na noti bandia. Aidha, kwa mujibu wa Kamanda Mtafungwa amesema kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa katika msako uliofanyika katika wilaya mbalimbali za mkoa huo na kubaini watuhumiwa hao wakiwemo 10 waliotekeleza mauaji kwa imani za kishirikina. Na dar24

Haya hapa Magazeti ya Tanzania March 23 2018

Image
Asubuhi nyingine tena na habari kubwa kwenye Magazeti ya Tanzania March 23 2018 kuanzia ya, Udaku, Michezo na Hardnews kujionea yote makubwa yaliyoandikwa

msuva ageuka lulu dau la usajili lapanda hadi........

Image
Msuva amejiunga na timu hiyo Julai 29, mwaka jana kwa dau la dola 150,000, sawa na zaidi ya Sh milioni 337 akitokea Yanga, lakini sasa ukitaka kumpata, Waarabu wanamthaminisha kwa euro 475,000, sawa na zaidi ya Sh bilioni 1.3. Mpaka sasa amefanikiwa kufunga mabao sita kwenye ligi ya nchi hiyo huku akifunga mabao manne katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Mbali ya mabao hayo, Msuva amefanikiwa kucheza mechi 16 za ligi na moja ikiwa ni ya Ligi ya Mabingwa Afrika hali iliofanya thamani yake kuongezeka. Kwa mujibu wa mtandao mmoja maarufu nchini Morocco ambao unahusika kutoa taarifa za thamani ya wachezaji, dau la Msuva sasa ni euro 475,000. Dau hilo ambalo limeonekana kupanda kwa Msuva, pia unaweza kusajili kikosi kizima cha Simba ambacho kilitajwa kuwa na thamani ya Sh bilioni 1.3. Kuongezeka kwa thamani ya mshambuliaji huyo, kumetokana na kuonyesha uwezo mkubwa kwenye ligi ya Morocco tangu ajiunge na timu hiyo akitokea Yanga msimu uliopita ambao aliondoka akiwa ni mfungaj

Raisi Magufuli azidi kugongelea msumari

Image

anyongwa hadi kufa na wasiojulikana

Image
Watu wasiojulikana MkoaniShinyanga wamemnyonga hadi kufa Salome Paschal (30) mkazi wa Kijiji cha Zunzuli katika Kitongoji cha Kituli, Kata ya Salawe wilayani Shinyanga na kisha kuutupa mwili wake kwenye kichaka. Akizungumza jana Jumapili Machi 18, 2018 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba, polisi wanaendelea kufanya uchunguzi kwa aliyehusika na mauaji ya hayo. Akisimulia tukio hilo, mume wa Salome aitwaye Isaya Mshomari amesema mkewe ameuawa Machi 17, 2018 saa nane mchana kwa maelezo kuwa alimuaga kuwa anakwenda sokoni kununua mahitaji ya nyumbani kisha aje awapikie wafanyakazi waliokuwa shambani. Na mwananchi

Haya hapa Magazeti ya Tanzania March 19 2018

Image
Kutana na habari kubwa kwenye Magazeti ya Tanzania March 19 2018 kuanzia ya, Udaku, Michezo na Hardnews kujionea yote makubwa yaliyoandikwa