Posts

Showing posts with the label BREAKING NEWS

BREAKING NEWS, ;Tundu Lissu amelionajuwa kwa marayakwanza

Image
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ametoka ICU na sasa anaweza kukaa. Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne, Mbowe amesema afya ya Lissu inaimarika kwa kuwa alihitaji upasuaji mwingi sana kutokana na risasi zilizoingia kwenye mwili wake. “Amefanyiwa upasuaji mkubwa mara 17 mpaka sasa. Ameongezewa damu nyingi kuliko mtu yeyote miaka 20 iliyopita ametoka ICU wiki iliyopita,” amesema Mbowe. Amesema Lissu hatumii oxygen tena wala mirija na kwamba anakula chakula anachokitaka. “Juzi kwa mara ya kwanza alikaa, anatembea Wheel Chair na aliliona jua kwa mara ya kwanza,” amesema Mbowe. “Tunawashukuru madaktari wa Dodoma na Nairobi. Hospitali ya Nairobi imefikisha awamu ya pili ya kutibu. Tunavyozungumza baada ya wiki moja kadri madaktari watakavyoshauri atamaliza matibabu ya pili,” “Ataanza awamu ya tatu nje ya Nairobi yatakayokuwa ya muda mrefu. Kwa usalama wake hatutataja wapi anakwenda. Siyo Tanzania na sio jiran...

BREAKING NEWS, TANGA polisi watumia mabomu kutawanya watu

Image
Madereva wote wa Hiace zinazofanya safari za Mjini kwenda Mikanjuni, Donge, Tanga Beach, Mwahako na Magomeni wameamua kugoma kutoa huda kwa kile wanachoita kunyanyaswa barabarani na kutozwa faini kwa uonevu pamoja na kusumbuliwa. Madereva hao wameamua kusimamisha kila Hiace iliyobeba abiria na kuwaamuru kushuka ndani ya gari. Kama inavyoonekana kwenye picha baadhi ya wanafunzi wakijaribu kutafuta njia mbadala ili waweze kufika shuleni. Habari zaidi nitwaletea kadri nitakavyo zipata. Daladala za mkoani Tanga zimegoma kufanya shughuli za usafirishaji jijini hapo na kujikusanya sehemu ya Komesho(mabawa), barabara ya Pangani kutokana na malalamiko yao kibao kutosikilizwa na serikali! Hivyo Jeshi la Polisi imebidi kutumia nguvu ya mabomu kuwatawanyisha eneo husika.. Najf

BREAKING NEWS, :auawa kwa kupigwa risasi

Image
Mkazi wa jijini Dar es Salaam, Robert Massawe (51), ambaye polisi wanadai ni mtuhumiwa wa uporaji na mauaji, ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaodaiwa kuwa ni wahalifu wenzake. Kabla ya kuuawa katika majibizano ya risasi, mtuhumiwa huyo anadaiwa alikamatwa akiwa na SMG yenye risasi 24, simu 19 zilizoporwa maeneo mbalimbali na laini za simu 58. Taarifa iliyotolewa leo Jumanne na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Issah imesema mtuhumiwa aliuawa na wenzake saa tisa usiku wa kuamkia jana wilayani Rombo. Amesema mtuhumiwa pamoja na mkewe walikamatwa jijini Dar es Salaam na baada ya kuhojiwa na polisi inadaiwa alieleza matukio ya ujambazi aliyoshiriki na alikubali kuwaonyesha mahali alipoficha bunduki. Polisi imesema simu tatu kati ya 19 wamegundua ziliporwa Moshi na moja alikuwa akiitumia mkewe ambaye anashikiliwa Dar es Salaam. Kamanda Issah amesema aliwaeleza polisi kuhusu mpango wa kufanya tukio la ujambazi katika Kijiji cha Chilio, Kata ya Holili wilayani Rombo...

BREAKING NEWS: Rais John Magufuli ametangaza mabadiliko ya baraza la mawaziri, baadhi wameachwa na wapya wametajwa.

Image
BARAZA LA MAWAZIRI: Mawaziri 21 - Zimeongezeka 2 Manaibu 21 - Zimeongezeka 5 Utumishi - George Mkuchika Nishati - Dkt. Medard Kalemani - Naibu Subira Mgalu Madini - Angela Kairuki - Naibu Stanslaus Haroon Nyongo Ujenzi - Prof Makame Mbarawa - Atashasta Nditie na Elias Kwandikwa Fedha - Dkt. Philipo Mpango - Dkt. Ashatu Kijaji Katiba - Palamagamba  Kabudi Habari - Dkt. Harrison Mwakyembe - Naibu Waziri - Juliana Shonza Ndani - Mwigulu Nchemba - Naibu Hamad Masauni Maliasili - Dk. Hamis Kigwangala -  Naibu Japhet Hasunga Ardhi - Willam Lukuvi - Naibu Angelina Mabula

BREAKING NEWS, :Alichokisema Mbowe kwa wanahabari

Image
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kwa sasa hakuna utaratibu wa kumsafirisha Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kwenda Marekani au Ujerumani kutokana na ushauri wa madaktari wanaomtibu. Akizungumza leo Ijumaa jijini hapa, Mbowe amesema madaktari wamesema hawezi kwenda popote kutokana na hali yake. Amesema baada ya awamu ya kwanza ya matibabu aliyoyapata katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma baada ya kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi Septemba 7, ya pili inafanyika Nairobi, Kenya alipo sasa. "Awamu ya tatu itaamua aende wapi ambayo itahusu mazoezi," amesema Mbowe.

BREAKING NEWSA: skari anayejiita Faru John amejisalimisha

Image
Askari anayejiita Faru John amejisalimisha kwa Kamanda wa Kanda Maalum DSM, Lazaro Mambosasa kutokana na agizo alilolitoa jana Mbagala Tutakjulisha zaidi

BREAKING: Mahakama ya Kisutu imemuachia huru Yusuf Manji

Image
Mfanyabiashara Yusuf Manji na wenzake watatu waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa kukutwa wakiwa na mabunda 35 ya vitambaa vinavyotumika kutengeneza sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) zenye thamani ya Sh milioni 192.5 wameachiwa huru baada ya kesi yao kufutwa na Mahakama ya Kisutu. Kesi hiyo imefutwa baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) kusema hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.   Na Jf

BREAKING NEWS:Jengo la ghorofa lavamiwa Dar

Image
Dar es Salaam. Watu wanane wanaodaiwa kuwa ni wahalifu wamevamia jengo la Prime House lililopo Mtaa wa Tambaza na kufanya uharibifu wa mali za wapangaji. Jengo la Prime House lina ghorofa tano lipo jirani na ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wilayani Ilala. Mwandishi wa gazeti hili ameshuhudia barabara ya kuingia eneo hilo ikifungwa kwa muda na polisi ambao walitumia magari yao kuziba njia na kuweka uzio wa utepe wa rangi ya njano. Jengo la Prime House lina ofisi za kampuni mbalimbali, zikiwemo za mawakili, duka la dawa na sehemu ya kufanya mazoezi gym . Mmoja wa mawakili ambao wana ofisi katika jengo hilo, ambaye hakutaka kutaja jina lake aliliambia gazeti hili kwamba watu hao walipofika walimfunga mlinzi kwa kamba na kisha kuingia ndani kwa nguvu. "Mlinzi ameniambia baada ya kuingia walipokuwa wakifanya upekuzi walikuwa wakisikika wakisema si huku tutazame ghorofa linalofuata si hili,” wakili huyo amemkariri mlinzi. Wakili huyo amesema, ...

BREAKING NEWS: Matokeo ya mtihani wa kidato cha sita 2017 yapo ...

Image
Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokoe ya mtihani wa kuhitimu elimu ya sekondari kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita.  Bonyeza  HAPA  kufatilia matokea ya shule zote Tanzania.