Posts

Showing posts from October, 2017

CCM CHADEMA wajibizana kwa maneno haya

Image
Moja ya habari kubwa za Tanzania leo October 30 2017 ni kujiuzulu kwa Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu ambae pia ametangaza kujiuzulu nafasi zake zote ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM. Baada ya kauli hiyo AzamTV imemuhoji Katibu Mkuu wa Itikadi na Uenezi CCM Humphrey Polepole ambae amesema “ Ni jambo la kawaida kabisa mtu ambae ameondoka anazo haki zote, wameondoka Wazito kwenye chama hiki na chama kimebaki kimoja kwahiyo huyu sio sehemu ya wazito, ni Mwananchi ambae ana haki ya kufanya hivyo “ “ Kwenye chama cha Mapinduzi kila kipindi ambacho tumekua tukifanya mageuzi makubwa ambayo yanatoa tafsiri pana ya kifikra na kuonyesha mwelekeo mpya, watu wengi huputika… nina uhakika wako kadhaa ambao wanashindwa kwenda na mwendokasi huu sasa kabla shoka halijawekwa shinani unakimbia mapema ” – Polepole CHADEMA kwa upande wake kimesema “ Chama cha siasa ni watu na hakuna chama cha siasa ambacho kitasema hatutaki watu, tunampongeza sana kwa uamuzi wake huo na ni uamuzi wa kiza

Magazeti ya Tanzania leo October 31 2017

Image
Magazeti ya Tanzania leo October 31  2017  kuanzia ya Dini, Michezo na Hardnews kujionea yote makubwa yaliyoandikwa

Hatimaye Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) yamtangaza Uhuru Kenyatta kuwa mshindi

Image
Hatimaye Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) imemtangaza Uhuru Kenyatta kuwa mshindi wa kinyang’anyiro cha urais baada ya kujikingia kura 7,483, 895 sawa na asilimia 98 katika uchaguzi wa marudio uliosusiwa na mpinzani wake mkuu, Raila Odinga. Kwa matokeo hayo, Rais Kenyatta na makamu wake William Ruto walikabidhiwa vyeti vya ushindi na sasa Uhuru anasubiri kuapishwa kuiongoza nchi kwa miaka mitano ikiwa matokeo hayo hayatapingwa na kufutwa. Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati alitangaza matokeo hayo bila kura kutoka majimbo 25 ya eneo la Nyanza ambalo wafuasi wa Odinga walifanya vurugu na kusababisha uchaguzi kuahirishwa. Chebukati alisema mazingira yaliyokuwa yameandaliwa kwa ajili ya uchaguzi wa marudio yaliwezesha kuwa wa kuaminika, huru na wa haki. Akizungumza mapema, Makamu mwenyekiti wa IEBC Consolata Nkatha alisema kura za maeneo ambayo hayakufanya uchaguzi hayawezi kuathiri matokeo ya mwisho. Uhakiki kura Nkatha alisema mchakato ulikamilika katika majimbo 266 ambako uch

Lazaro Nyalandu: Ajivua uanachama ccm

Image
NIMEAMUA kujiuzulu NAFASI yangu ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, pamoja na nafasi zote za Uongozi ndani ya Chama kuanzia leo, Oktoba 30, 2017. HALIKADHALIKA, asubuhi ya leo nimemwandikia Spika wa Bunge, Mh. Job Ndugai, Mb., barua ya kujiuzulu nafasi yangu ya UBUNGE wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia tiketi ya CCM, nafasi ambayo nimeitumikia kwa vipindi vinne mfululizo tangu nilipochaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2000 hadi Sasa. AIDHA, Nimechukua UAMZI huo kutokana na kutorishwa kwangu na mwenendo wa hali ya Kisiasa nchini, ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa HAKI za Kibinadamu, ongezeko la vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa baadhi ya watanzania wenzetu, na kutokuwepo kwa mipaka ya wazi kati ya MIHIMILI ya dola (Serikali, Bunge, na Mahakama) kunakofanya utendaji kazi wa Kibunge wa Kutunga Sheria na wa Kuisimamia Serikali kutokuwa na uhuru uliainishwa na kuwekwa bayana KIKATIBA. VILEVILE, Naamini kwamba bila Tanzania kupata Katiba Mpya Sasa, hakuna na

maendeleo ya Tundu lissu mpaka sasa

Image
Lissu anatibiwa jijini Nairobi nchini Kenya mara baada ya kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi na watu wasiojulikana, septemba 7 akiwa mkoani Dodoma akitoka kuhudhuria vikao vya Bunge. “ Kwa sasa nipo Arusha, ila tangu nilipotoka hivi karibuni Nairobi alikuwa anaendelea vizuri na hali yake inazidi kuimarika na anaendelea na mazoezi kila siku, unajua chumba alichomo kwa sasa ni kikubwa, hivyo anafanya mazoezi humo humo ,”amesema Mughwai Aidha, tangu septemba 7, Lissu hakuwahi kuonekana hadharani hadi oktoba 18 zilipotolewa picha zake na kutumwa kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha akiwa amelala kitandani na zingine zikimuonyesha akiwa kwenye kiti cha magurudumu. Hata hivyo, ameongeza kuwa kuhusu kutibiwa nchi za nje, amesema kuwa taarifa ataitoa pale muda utakapo wadia hivyo amewaomba Watanzania kuwa wavumilivu kwani taratibu zinafanyika.

Miaka 24 Jela Kwa Kuambukiza Ukimwi Wanawake 30

Image
Mwanaume mmoja nchini Italia ambaye pia ni muathirika wa UKIMWI, amehukumiwa miaka 24 jela kwa kuambukiza virusi vya ugonjwa huo wanawake takriban 30, licha ya kujua hali yake. Mwanaume huyo aliyejulikana kwa jina la Valentino Talluto mwenye umri wa miaka 33, alikuwa akiwashawishi wanawake hao kufanya nao ngono bila kujikinga, kwa madai kwamba amepima karibuni na ana 'allerg' na condom. Valentino alikuwa akiwapta wanawake hao kwa kutumia mitandao ya kijamii na kuwarubuni, huku akiwa na mahusiano na wanawake zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja. Waendesha mashtaka wa mjini Roma Italia, waliomba apewe kifungo cha maisha jela, lakini baada ya majadiliano ya masaa 12 mahakama iliamua kumfunga miaka 24 jela. Akiwa mahakamani Talluto alielezea kujuta kwake kwa kufanya kitendo hicho, na kusema kwamba hakujua madhara ya vitendo hivyo. Wanawawake wengi walikutwa na HIV kutokana na matatizo ya kiafya baada ya kufahamu juu kukamatwa kwa Talluto, na miongoni mwa wanawake hao mmoja n

MBUNGE wa Nzega Mjini, Hussein Bashe ajitolea kwa wazee

Image
MBUNGE wa Nzega Mjini, Hussein Bashe, ametoa vitambulisho vya matibabu bure kwa wazee 3,284 wa jimbo lake huku akisema amefanya hivyo kwa kuwa wazee hao wamelitumikia Taifa kwa muda mrefu na sasa ni vyema vijana wakawahudumia. Utoaji wa vitambulisho hivyo ni utekelezaji wa Sera ya Taifa Matibabu ya Bure kwa wazee, ambapo baada ya kupata vitambulisho hivyo, itakuwa rahisi kwao kwenda hospitali na kupatiwa matibabu bila malipo. Katika uzinduzi wa zoezi hilo, Bashe ametoa vitambulisho 540 na vingine vitaendelea kutolewa katika ofisi ya Mbunge iliyopo Nzega Mjini. Akizungumza na wazee waliojitokeza kupokea vitambulisho hivyo, Bashe alisema: “Wazee hawa wameitumikia nchi hii kwa muda mrefu, ni jukumu letu sasa kama vijana na Taifa kuhakikisha nasi tunawalipa sehemu ya nguvu kubwa walizotumia kuifikisha Tanzania hapa ilipo leo kwa kuwapatia matibabu bora na kuwaondolea gharama za matibabu ili kuleta unafuu wa maisha. “Nilichokifanya ni kugharamia fedha zote za vitambulisho ili kuhakik

Magazeti ya Tanzania leo October 30 2017

Image
Magazeti ya Tanzania leo October 30  2017  kuanzia ya Dini, Michezo na Hardnews kujionea yote makubwa yaliyoandikwa