maendeleo ya Tundu lissu mpaka sasa

Lissu anatibiwa jijini Nairobi nchini Kenya mara baada ya kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi na watu wasiojulikana, septemba 7 akiwa mkoani Dodoma akitoka kuhudhuria vikao vya Bunge.
Kwa sasa nipo Arusha, ila tangu nilipotoka hivi karibuni Nairobi alikuwa anaendelea vizuri na hali yake inazidi kuimarika na anaendelea na mazoezi kila siku, unajua chumba alichomo kwa sasa ni kikubwa, hivyo anafanya mazoezi humo humo,”amesema Mughwai
Aidha, tangu septemba 7, Lissu hakuwahi kuonekana hadharani hadi oktoba 18 zilipotolewa picha zake na kutumwa kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha akiwa amelala kitandani na zingine zikimuonyesha akiwa kwenye kiti cha magurudumu.

Hata hivyo, ameongeza kuwa kuhusu kutibiwa nchi za nje, amesema kuwa taarifa ataitoa pale muda utakapo wadia hivyo amewaomba Watanzania kuwa wavumilivu kwani taratibu zinafanyika.

Comments


Popular posts from this blog

ILE SINTOFAHAMU YA NANI BINGWA WA VPL HII HAPA

Michezo:Ajibu huyo yanga

ELIZABETH MICHAEL ' LULU' awafungukia wasanii wa bongo move

fahamu kilichojiri nyumbani kwa Tundulisu