Posts

Showing posts from August, 2017

TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMISI 31.08.2017

Image
Arsenal wanafanya jaribio la dakika za mwisho kumsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain Julian Draxler, 23, na wakimkosa watazuia uhamisho wa Alexis Sanchez, 28, kwenda Manchester City. (Daily Mirror) Manchester  City watapanda dau la pauni milioni 70 taslimu kutaka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28, na tayari wamepeleka kikosi chake cha wansheria na madaktari nchini Chile kwa ajili ya kukamilisha usajili huo. (Independent) Matumaini ya Manchester City ya  kumsajili beki wa West Brom Jonny Evans, 29, bado ni ati ati, kwa sababu Eliaquim Mangala, 26, ambaye angehusika katika mkataba huo hataki kwenda West Brom. Arsenal na Leicester walipanda dau la pauni milioni 25 kumtaka beki huyo, lakini maombi yao yalikataliwa. (Daily Telegraph) Crystal palace wana matumaini ya kumsajili Eliaquim Mangala kutoka City kwa pauni milioni 23. (Sun) Swansea wanakaribia kumsajili kiungo wa Bayern Munich Renato Sanches kwa mkopo. (Guardian) West Ham wanapanga kumchukua Jack

Mgogoro mwingine Chadema na serikali

Image
Katika kikao alichofanya na wanahabari, Mwenyekiti wa CHADEMA, Halmashauri ya mji wa Tunduma, Ali Mwafongo ameleezea kusikitishwa na amri hiyo ya mkuu wa wilaya na kusema kuwa kamwe hawatarudi nyuma huku akiahidi kutompa ushirikiano mkuu wa wilaya huyo. “Uchungu tunaopata sasa hivi tunajua ipo siku itakuwa furaha kwetu kwani ushindi unakaribia. Kinachofanywa sasa hivi wakumbuke ipo siku watawala watakuwa wapinzani na haya yanayofanywa hayataweza kuturudisha sisi nyuma. Viongozi wetu wamekuwa wakipelekeshwa sana lakini katu hatutokata tamaa kwa sababu ni kazi yetu kusema ukweli na kuwatumikia wananchi wetu ” alisema Mbali na hayo mkuu huyo wa wilaya pia ametuhumiwa kutoa amri ya kushusha bendera za chama hicho hali ambayo imeonesha kuwakera baadhi ya viongozi wakiwemo madiwani. Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo, Juma Irando amekiri kutoa amri ya kukamatwa kwa mbunge huyo kwa madai kuwa ametoa kauli ya kudharau mamlaka ya uteuzi. Mbunge Mwakajoka amekamatwa Jumanne na kuwekwa nda

Mahanga akamatwa na Polisi

Image
Dar es Salaam. Mbunge wa zamani wa Ukonga na Segerea, Dk Makongoro Mahanga amekamatwa na Polisi Mkoa wa Ilala kwa amri ya Mahakama Kuu na amefikishwa mahakamani. Mahakama iliamuru Dk Mahanga akamatwe na kufikishwa mahakamani kwa kushindwa kutekeleza uamuzi unaomtaka amlipe mdai Kainerugaba Msemakweli Sh14 milioni. Fedha hizo ni gharama za kesi alizozitumia Msemakweli baada ya kushinda kesi ya madai ya kashfa ambayo Dk Mahanga alimfungulia kwa kumtaja kwenye kitabu chake kinachoitwa: “Mafisadi wa Elimu”. Katika kitabu hicho anamtaja kuwa ni mmoja wa viongozi wenye shahada za udaktari wa kughushi. Kati ya kiwango hicho cha fedha, Dk Mahanga ameshalipa Sh6 milioni hivyo anadaiwa Sh8 milioni.  Na mwananchi

Magazeti ya Tanzania leo August 31 2017 kuanzia ya Udaku, Michezo na Hardnews

Image
 Ni asubuhi nyingine tena nakukutanisha na habari kubwa kwenye Magazeti ya Tanzania leo August 31  2017  kuanzia ya Udaku, Michezo na Hardnews kujionea yote makubwa yaliyoandikwa.

Lema afunguka haya kuhusu utekaji wa watoto

Image
Mh. Lema amesema matukio hayo ni mabaya na kwamba yanaleta taharuki na huzuni kwa wazazi na walezi hivyo ni vyema polisi wakachukua hatua za haraka kuwabaini watu wanaotekeleza vitendo hivyo na kuvikomesha. Mbunge huyo amesema watekaji hao mara baada ya kuwateka watoto wanadaiwa kutoa barua za madai ya fedha kwa kificho ili wawaachie watoto na kwamba, endapo madai yao hayatakelezwa hutishia kuwaua. Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Olkerian, Daudi Safari, amesema wasiwasi umezikumba familia nyingi kufuatia matukio hayo hali iliyosababisha wazazi na walezi kushindwa kutekeleza majukumu yao mengine wakitumia muda mwingi kuwalinda watoto wao. Mpaka sasa watoto wanaodaiwa kutekwa nyara ni Maurine David, Ikram Salim, Ayoub Fred Bakari Salim. Juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha kuzungumzia matukio hayo zimegonga mwamba

Jux afunguka haya kuhusu vanessa mdee

Image
Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Jux amesema Vanessa sasa hivi yupo kwenye wakati mgumu katika kufanya mambo yake ya kawaida, hivyo ni jukumu lake kuhakikisha haeleweki vibaya mbele za watu. “Kuna vitu mimi siwezi kuvifanya ili kumlinda na yeye hawezi kufanya kunilinda mimi, japo watu watasema vingi hasa kwa mwanamke pale anapoamua kufanya baadhi ya vitu vyake binafsi. Natakiwa kumlinda Vanessa sasa hivi kwa kuwa kila jambo ambalo atalifanya watu watamfikilia vibaya hivyo napaswa kumlinda kutokana na hilo kwa sababu wanawake wenyewe wako wachache”, alisema Jux. Jux aliendelea kwa kusema kuwa wakati bado wako kwenye mahusiano Vanessa alikuwa na uhuru wa kufanya jambo lolote, kwani karibia kila mmoja aliamini yupo na Jux ndiye mtu wake. “Muda mwingine anaweza akashindwa hata kufanya vitu vingine, mwanzo hata akionekana na mtu wana-shoot au wanafanya nini, wanajua yupo na Jux, lakini sasa hivi hawezi”, alisema Jux Pia Jux aliweka wazi kuwa ingawa bado ana kidon

, Tundu Lissu akiwa sambamba na Dkt. HEllen Kijo-Bisimba

Image
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Tundu Lissu akiwa sambamba na Dkt. HEllen Kijo-Bisimba ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na baadhi ya mawakili wanaounga mkono wito uliotolewa na Tundu Lissu wa kuwataka mawakili wote kugomea kufika Mahakamani kutekeleza majukumu yao ya kisheria ikiwa ni kuonyesha msimamo wao wa kupinga kitendo cha jengo la mawakili wa IMMA kulipuliwa kwa kile kinachodhaniwa kuwa ni bomu la petroli. Hata hivyo, wito huo haukuitikiwa na mawakili wengi kama ilivyotarajiwa na Tundu Lissu kwani wengi walifika kusikiliza kesi zinazowahusu katika mahakama mbalimbali nchini. "Sio kwamba sisi hatujaguswa na kilichowapata wenzetu wa IMMA Advocates isipokuwa hili la Rais wao Tundu Lissu ni kuchanganya mambo mawili yasiyohusiana kwani kuchomwa kwa ofisi tayari Polisi wanafanya uchunguzi na hawajatoa majibu na hiyo ni Taasisi iliyo chini ya Serikali ambapo Mahakama ni mhimili unaojitegemea hauingiliani kimajukumu

Young Dee Afunguka Kumsweka Rumande Amber Lulu Kisa Picha za Utupu

Image
Msanii wa muziki kutoka King Cash, Young Dee amedai tayari ameshamchukulia hatua za mwanzo muimbaji na video vixen, Amber Lulu baada ya kumtuhumu kuwa yeye ndiye aliyesambaza picha chafu mtandaoni zinazomuonyesha msichana huyo akiwa mtupu huku rapa huyo akimshika makalio. Bongo5 ilimtafuta rapa huyo na kuzungumza naye sababu na kupiga picha hizo na madhara yaliyojitokeza baada ya kusambaa.

Wimbo ‘Seduce Me’ wa Alikiba umevunja hii rekodi

Image
Staa Alikiba amekuwa miongoni mwa wasanii waliovunja rekodi ya kufikisha views Millioni Moja kwenye YouTube ndani muda mchache tu tangu kuachia video yake ya wimbo ‘Seduce me’. Baada ya kuvunja rekodi hiyo Alikiba ametoa shukrani kwa mashabiki kupitia Instagram yake kwa kuandika>>> “Ahsanteni sana. Thank you for the love, I couldn’t be more blessed and favoured. You mean a lot to me and I do this for YOU. Nawapenda sana #RockstarTV #SHOOOOSH#SonyMusicAfrica #RockStar4000#KingKiba“

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAPILI 27.08.2017

Image
Liverpool wameweka makataa ya hadi Jumatatu, kwa Barcelona wawe wamefikia bei ya Philippe Coutinho, 25. (Onda Cero) Liverpool wanataka kukamilisha usajili wa  Alex Oxlade Chamberlain, 24, kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Chelsea pia wanamtaka winga huyo wa Arsenal. (Sunday Mirror) Mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28, imeripotiwa anaitaka klabu yake kumfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika EPL iwapo wanataka asaini mkataba mpya. (Daily Star) Meneja wa Arsenal Arsene Wenger hajakata tamaa ya kumsajili Thomas Lemar wa Monaco, 22,  pamoja na Virgil van Dijk, 26, ingawa huenda ikawa msimu ujao. (Sun) Arsenal wanataka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Marco Asensio, 21. (Sunday Express) Paris Saint-Germain wanaendelea na majadiliano ya kumsajili mshambuliaji wa Monaco Kylian Mbappe kwa pauni milioni 166 kabla ya dirisha la usajili kufungwa, ingawa Monaco wenyewe wanataka Mbappe aende Real Madrid. (Sunday Telegraph) Iwapo Kylian Mbappe ataondoka Monaco, klabu

Jeshi la Polisi Arusha lazuia mikutano ya Lema

Image
Jeshi la polisi mkoani Arusha, limepiga marufuku mikutano ya mbunge wa jimbo la Arusha mjini (Chadema), Godbless Lema iliyokuwa inaendelea katika jiji la Arusha ili kupisha maandalizi ya mtihani wa darasa la saba na mbio za Mwenge. Katika barua ya Mkuu wa polisi wilaya ya Arusha, Mrakibu mwandamizi wa polisi (SSP),E.Tille ambayo imethibitisha na Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha,(SACP) Charles Mkumbo imeeleza kuwa, Lema amezuiwa kufanya mkutano kuanzia kesho Agosti 27 hadi Septembaa mosi. “Ofisi ya Mkuu wa polisi wilaya ya Arusha, inakutaarifu kuwa imezuia mikutano yako yeye ratiba kuanzia Agosti27 hadi Septema mosi kwa ajili ya kupisha maandalizi ya kuhitimisha mtihani wa darasa la saba na mwenge wa uhuru” ilisomeka barua hiyo na kushauri Lema kupanga mikutano kuanzia Septemba 8 mwaka huu. Kamanda Mkumbo amesema, sababu kubwa ya kuzuiwa mikutano hiyo ni kwa kuwa wanahitajika polisi wa ulinzi na hivyo haiwezekani kupata polisi wa kulinda mikutano na pia kushiriki katika masuala ya

LWANDAMILA ALAMBA SHAVU NONO TOKA YANGA

Image
KIROHO safi Yanga imeamua kumuongezea mkataba wa mwaka mmoja kocha wake George Lwandamina raia wa Zambia baada ya ule wa awali kumalizika Julai 16, mwaka huu. Katika mkataba wake uliopita, Lwandamina aliiwezesha Yanga kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita na kuifikisha katika nusu fainali ya Kombe la FA kabla ya kutolewa na Mbao FC ya Mwanza. Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa aliliambia Championi Jumamosi jana mchana kuwa, wameamua kumuongezea mkataba Lwandamina baada ya kuridhishwa na kazi yake. “Tunaingia mkataba mwingine wa mwaka mmoja na Lwandamina kwani ule wa mwanzo umeisha na sasa kila kitu kipo tayari hivyo muda wowote tena kwa uwazi kabisa atasaini mkataba mpya. “Tumejitahidi kwa uwezo wetu kuboresha mkataba wake mpya kwa kumuongezea maslahi kidogo ili apate motisha ya kufanya kazi yake ipasavyo,” alisema Mkwasa. Lwandamina alitarajiwa kusaini mkataba huo muda wowote kuanzia jana mchana ili awe na uhakika wa kuendelea kufanya kazi yake kwa uhuru na

Magazeti ya Tanzania leo August 27 2017 kuanzia ya Dini, Michezo na Hardnews

Image
Ni asubuhi nyingine tena nakukutanisha na habari kubwa kwenye Magazeti ya Tanzania leo August 27  2017  kuanzia ya Dini, Michezo na Hardnews kujionea yote makubwa yaliyoandikwa.