LWANDAMILA ALAMBA SHAVU NONO TOKA YANGA

KIROHO safi Yanga imeamua kumuongezea mkataba wa mwaka mmoja kocha wake George Lwandamina raia wa Zambia baada ya ule wa awali kumalizika Julai 16, mwaka huu. Katika mkataba wake uliopita, Lwandamina aliiwezesha Yanga kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita na kuifikisha katika nusu fainali ya Kombe la FA kabla ya kutolewa na Mbao FC ya Mwanza.

Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa aliliambia Championi Jumamosi jana mchana kuwa, wameamua kumuongezea mkataba Lwandamina baada ya kuridhishwa na kazi yake.

“Tunaingia mkataba mwingine wa mwaka mmoja na Lwandamina kwani ule wa mwanzo umeisha na sasa kila kitu kipo tayari hivyo muda wowote tena kwa uwazi kabisa atasaini mkataba mpya.


“Tumejitahidi kwa uwezo wetu kuboresha mkataba wake mpya kwa kumuongezea maslahi kidogo ili apate motisha ya kufanya kazi yake ipasavyo,” alisema Mkwasa. Lwandamina alitarajiwa kusaini mkataba huo muda wowote kuanzia jana mchana ili awe na uhakika wa kuendelea kufanya kazi yake kwa uhuru na kujiamini.

Comments


Popular posts from this blog

wananchi wamshtaki polisi kwakuwanyanyasa

sharti la polepole lapata upinzani

KENYA:Tume Huru ya Uchaguzi yaridhia maombi ya upinzani

Angelina Jolie kuonekana kwenye jarida la ‘Vanity Fair’.

Afisa wa serikali ajinyonga

Viongozi wa G7 waangazia bara la Afrika

UEFA kuendelea kutimuavumbi hii leo

YANGA YASHUSHA STRAIKA WA AFCON