Posts

Showing posts from July, 2017

Meneja wa tume ya uchaguzi aliyetoweka Kenya apatikana amefariki

Image
Afisa wa cheo cha juu wa tume ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya IEBC, ambaye alitoweka siku ya Ijumaa amepatikana akiwa amefariki. Mwili wa Christopher Chege Musando, ambaye alikuwa kaimu mkurugenzi wa masuala ya teknolojia wa IEBC, umepatikana kwenye chumba kimoja cha kuhifadhi maiti jijini Nairobi Mawasiliano ya mwisho kutoka mwa Musando aliyafanya siku ya Jumamosi mwendo wa saa tisa alifajiri kupitia ujumbe wa SMS kwa mmoja wa wafanyakazi wenzake. Na BBC

Tamko la Kamati ya Chadema

Image
Tumekuwa tunafanya uchumi wa matukio, kurukia rukia matukio Makinia limezikwa, tupo kweye Tegeta Escrow na IPTL  - Kama wabunge wa pande zote mbili wangekuwa na msimamo hii bajeti ya serikali ya 2017/2018 isingepita 'Fedha zililizopelekwa kununua ndege zingepelekwa kwenye kilimo kuna Watanzania zaidi ya milioni 40 wangecheka' - Kiwanda kilichokuwa kinazalisha ndara mwaka 1962 hakiwezi kuendelea kuzalisha ndara zile zile kwa dunia ya sasa - Kilichofanywa kwenye makinia ni papara, wabunge CCM wakafanya papara hata Rais amefanya papara  na tumelishwa uongo- Mbowe Deni la nje kwa sababu tumeshindwa kuzalisha ndani ili serikali ijiendeshe lazima tukope, hawa watu wanakopa mno Sekta ya viwanda toka Magufuli ameingia madarakani vimekopa asilimia 0% kwa mujibu wa takwimu za BoT 'Hakuna mfanyabiashara duniani ambaye atapewa kitega uchumi kinachomuingizia faidi akakifunga' 'Viwanda vingi vilivyobinafsishwa vilikuwa vinaendeshwa kwa hasara, ni viwanda amba

WATUMISHI 400 WENYE ELIMU YA DARASA LA SABA SERIKALINI KUFUKUZWA KAZI

Image
Zaidi ya Wafanyakazi 400 wa Serikali wanatarajia kuondolewa kazini mkoani Morogoro kutokana na kushindwa kujienmini deleza kielimu baada ya kuajiriwa miaka 13 iliyopita wakiwa na vyeti vya elimu ya msingi. Watumishi hao ambao wengi wao ni wauguzi, wahudumu wa afya, madereva, wahudumu wa ofisi, watendaji wa mitaa, vijiji na kata tayari wamenyimwa mishahara yao ya mwezi huu. Akizungumzia zoezi hilo aliyekuwa Mtendaji wa Kata ya Kimamba wilayani Kilosa, Mashaka Motile amesema katika wilaya hiyo watumishi zaidi ya 80 wamenyimwa mshahara bila maelezo yoyote na walipofuatilia ndipo walipofahamishwa kuwa walipewa muda wa kujiendeleza na wameshindwa kufanya hivyo. “ amesema. Motile anasema yeye na baadhi ya watendaji wengine walisimamishwa kazi kimakosa kwani agizo linasema wasimamishwe kazi walioajiriwa kuanzia Mei 20, 2004 lakini wao waliajiriwa Mei Mosi, 2004. Akizungumzia uamuzi huo wa Serikali, mhudumu wa afya wa manispaa ya Morogoro ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema uamuz

SABABU YA KUWAKAMATA WAFANYAKAZI WA ACACIA HII HAPA

Image
Idara ya Uhamiaji   imesema jukumu la Udhibiti wa Uingiaji na Utokaji wa raia wa kigeni nchini, linatekelezwa kwa mujibu wa Sheria ya Uhamiaji Sura ya 54 (Rejeo la 2016) na wala haiwalengi wafanyakazi wa Kampuni ya Madini ya Acacia peke yake. Ni hitajio la kisheria kwa kila raia wa kigeni anayeingia na kutoka nchini kukaguliwa ili kujiridhisha iwapo hakuna dosari zozote za Uhamiaji, Ulinzi na Usalama. Sheria ya Uhamiaji inaitaka Idara ya Uhamiaji kumhoji mtu yeyote awe raia wa Tanzania au kigeni bila kujali anafanya kazi kwenye Kampuni au Shirika gani, pale inapotaka kujiridhisha juu ya uhalali wa ukaazi wake hapa nchini na ikijiridhisha kuwa mtu huyu hana dosari zozote inamwachia huru kama ilivyofanyika kwa wafanyakazi wa Kampuni ya Madini ya Acacia waliohojiwa na kuruhusiwa kuendelea na safari yao hivi karibuni. Idara ya Uhamiaji inapenda kuuarifu Umma kuwa hakuna sababu zozote nje ya matakwa ya Sheria  ya Uhamiaji zinazopelekea Idara ya Uhamiaji kuweka kizuizi  cha kuja au kuto

MANARA AMKABIDHI JPM KIWANDA

Image
Mkuu wa habari na mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara amemuonesha Rais Magufuli kiwanda kingine ambacho amedai kuwa ni kikubwa kuliko viwanda vyote nchini kinachoweza kusaidia utekelezaji wa kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano ya kujenga Tanzania ya viwanda. Kiwanda hicho ni mchezo wa soka, ambapo Manara amesema endapo kitafanyiwa uwekezaji wa kutosha kitaweza kuzalisha ajira nyingi kuliko viwanda vyo ambavyo serikali ya awamu ya tano imepanga kuvijenga na kuviendeleza. “TFF wanatakiwa waje na mpango wa kukiboresha na kukiunda kiwanda hiki sasa, maana mimi naona kama vile kiwanda hiki hakipo, serikali iwekeze kwenye football kuanzia chini. Kama Rais ameingia mahali, nchi nzima inatumia mashine za EFD, TRA makusanyo yameongezeka, ofisini kuna nidhamu ya kazi kwenye taasisi za umma, mambo yanakwenda, nakuhakikishia Rais akiingia hapa kwenye mpira, akaja kutuundia hiki kiwanda, ataacha legacy ambayo hajaacha Rais yeyote, na kisiasa itamsaidia sana katika uchaguzi

Wanawake wasiowaita waume kwa majina yao India

Image
Mamiloni ya wanawake nchini India hawajawai kuwaita mabwana zao kwa kwa majina yao ikiwa ni njia ya kuwaheshimu. Tamaduni hiyo inaheshimika zaidi vijijhini licha kutokuwepo saana mijini. Sasa waendesha kampeni wanawashauri wanawake vijijini paia nao waachane na tamaduni hiyo. "Wazazi wangu walioana kwa miaka 73 hadi babangu alipoaga dunia mwaka uliopita.     Na bbc

MWANZILISHI KAMPENI YA 'MAGUFULI BAKI' AKIMBILIA TCRA

Image
Mamalaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeombwa kufuatilia kwa makini  mawasiliano ya simu za mkononi ili kubaini watu wanaotumia mitandao hiyo  kinyume na sheria. Ombi hilo limetolewa na mwanaharakati Lawrence Mabawa  jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari vitisho anavyopata kupitia simu ya mkoni baada ya kutambulisha kampeni yake ya ‘BAKI MAGUFULI’. Kwa mujibu wa Mabawa, baadhi ya wananchi wameelewa vibaya kampeni hiyo na kufikia hatua ya kutoa maneno ya matusi na kejeli kwake. Akifafanua lengo la kampeni yake, Mabawa amesema alimaanisha kuwa Rais abaki na msimamo wake ambao kwa kiasi kikubwa unapeleka taifa la Tanzania mbele kimaendeleo, na si kama ambavyo watu hao wameichukulia.    Na Azamtv

Magazeti ya TZ leo July 31.. Udaku, Michezo na Hardnews

Image

Barnaba ammwagia sifa Dogo Aslay

Image
Kupitia kipindi cha eNewz cha EATV Barnaba alisema anafurahishwa na jinsi nyimbo za Aslay zinavyopendwa na kupenya sana uswahilini bila msanii huyo kutumia nguvu kubwa ya kiki au 'interview' nyingi. "Aslay yupo sawa kabisa, kitu kizuri ni kwamba mashabiki wanaongea wenyewe, uswahilini nyimbo zake zinapendwana sana na kwa sasa yeye ndiye msanii anayefanya vizuri kwa upande wangu" - Barnaba Classic Aidha Barnaba alisema Aslay anaandika stori nzuri sana huku akiwakumbusha wasanii wakubwa kuangalia anachokifanya msanii huyo na kujifunza. "Napenda sana anachokifanya Aslay, kwanza anaandika stori nzuri sana, mfano wimbo wake 'Mhudumu', au 'Danga' hata 'Ndoa" aliyomshirikisha Khadija Kopa" aliongeza msanii huyo. Aslay alikuwa mmoja wa wasanii waliounda kundi la Yamoto Band ambapo kwa sasa anafanya kazi zake mwenyewe, tangu aanze kufanya kazi nje ya kundi Aslay ameshaachia nyimbo kama 'Angekuona', 'Usiitie Doa', '

Mbunge Gulamali aelezea Sababu za kufufuliwa kiwanda cha ‘Manonga Ginery’

Image
Mbunge wa Jimbo la Manonga kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Seif Khamis Gulamali leo ametembelea kiwanda cha Manonga Ginery kinachohusika na kutengeneza pamba, kilichokuwa kimesimama kwa takribani miaka ishirini (20) bila ya kufanya kazi. Mapema leo hii Mbunge Gulamali aliwasili katika eneo la kiwanda hicho, iliyopo Jimbo la Manonga Kata ya Choma akiwa pamoja na Mmiliki wa kiwanda hicho, ndugu Urvesh Rajan pamoja na viongozi wa Serikali za mitaa, wahandisi na mafundi wa viwanda. Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea na kuona maendeleo ya ufufuaji wa kiwanda hicho ili kianze kufanya kazi upya, baada ya kukaa kwa miaka kadhaa bila ya kufanya kazi, Mbunge Gulamali alisema, leo nimekuja kuoana maendeleo ya kufufuliwa wa kiwanda hichi ikiwa ni sehemu ya kutaka kutimiza tena ahadi yangu niliyo itoa kwa wanachi wa Igunga na Manonga kwamba lazima kiwanda cha Manonga Ginery, kianze kazi ili wananchi waweze kunufaika katika zao biashara ya pamba na wengine kupata ajira kw

Daraja refu zaid duniani lazinduliwa

Image
Daraja lililotundikwa lenye mita 500 linalokisiwa kuwa refu zaidi duniani limefunguliwa katika mji wa Zermatt nchini Uswizi. Daraja hilo lenye urefu wa mita 494 kwa jina Europabrucke limetundikwa mita 85 juu . Bodi za utalii ya Zermatt inasema kuwa ndio daraja refu zaidi duniani ,ijapokuwa daraja la mita 405 mjini Reutte Austria limetundikwa mita 110 juu kutoka ardhini. Daraja hilo linachukua mahala pa daraja jingine ambalo lilikuwa limeharibiwa na mwamba. Daraja hilo jipya ambalo ambalo lina uzito wa tani nane limewekwa kifaa cha ambacho linalizuia kuyumbayumba ,kulingana na bodi ya watalii ya Zermatt. Daraja hilo lipo kati ya Zermatt na Grachen kusini mwa Switzerland.

Neymar mbioni kutua Psg

Image
Mshambuliaji wa Barcelona Neymar, 25, amekubali kusaini mkataba wa miaka mitano kujiunga na Paris Saint-Germain na huenda akakamilisha uhamisho wa pauni milioni 197 wiki ijayo. (RMC) PSG watawapa Barcelona Angel Di Maria, 29, kama sehemu ya mkataba wa kumsajili Neymar, ili kupunguza kodi ya kutengua kifungu cha uhamisho cha mchezaji huyo wa Brazil. (AS) Iwapo Neymar ataondoka, Barcelona wataamua kuwawinda wachezaji watatu kutoka EPL- Philippe Coutinho, 25, wa Liverpool, Eden Hazard, 26, wa Chelsea, na Delle Alli, 21 wa Tottenham kuziba pengo. (Mirror) Barcelona wana wasiwasi kuwa bei kubwa ya kumsajili Philippe Coitinho kutoka Liverpool huenda ikawakatisha tamaa. (AS) Kiungo wa Barcelona Andres Inisesta, 33, amesema ni Neymar pekee anayeweza kuzungumzia kuhusu hatma yake, akisema hadhani kama euro milioni 200-300 zina manufaa yoyote kwa klabu bila Neymar mwenyewe. (Marca) Monaco wanasisitiza kuwa hawatamuuza Thomas Lemar, 21, licha ya Arsenal kupanda dau la tatu la takriban paun

Magazeti ya TZ leo July 30.. Dini, Michezo na Hardnews

Image