NIANZE kwa kumpa pole sana mama wa watoto watano, Zarinah Hassan ‘The Bossy Lady’ ambaye wiki chache zilizopita, alipata msiba mkubwa baada ya kufiwa na baba wa watoto wake watatu wakubwa, Ivan ‘Don’ Ssemwanga. Kwa namna yoyote, ule ni msiba mkubwa mno, hasa unapomkuta mwanamke, kwani inaonyesha wanaume, licha ya nao kuwa na moyo wenye damu unaoonja maumivu, angalau ni wavumilivu kidogo, wanaweza kujikaza na kusahau ndani ya muda mfupi. Zari, licha ya kuwa ni shemeji yetu, lakini pia ni mtu ambaye anaonyesha jinsi gani mwanamke anapaswa kuwa mtafutaji badala ya kumtegemea mwanaume kama dada zetu wengi walivyo. Ni mbunifu katika mipango ya kupata mkwanja, tena ule wa maana. Ameonyesha hivyo mara nyingi, kwani kwa muda mchache ambao amekuwa ‘mtu wetu’, amejidhihirisha kuwa ni wa tofauti na mastaa wetu ambao ujanja wao mwingi unategemea pochi za wanaume. Kuna ile Zari White Party, ni moja ya matukio machache kubuniwa na mdada huyo na kufanikiwa, likifanyika pale Mlimani City, miak...
Comments