Posts

Showing posts with the label Mapenzi

Mwanamke anahitaji vitu hivi kutoka kwa mwanamume

Image
Kutatuliwa Matatizo Wanawake wengi hutegemea kuwa wanapokuwa na wapenzi watasaidiwa katika matatizo ya kimaisha na migogoro ya kimawazo. Kwa mfano ushauri juu ya maisha yao, kulindwa na hatari za kimaisha, kusaidiwa katika shida na kuongozwa pale wanapohisi kushindwa kufanya jambo. Kama mwanaume hatamfanyia mpenzi wake hili atakuwa amekosa sifa za kuteka penzi la mwanamke. Kubembelezwa Wanawake hupenda kubembelezwa pale wanapokuwa na huzuni, wengi wao hawapendi kukaripiwa, mara nyingi hupenda kuungwa mkono wanapokuwa na misuguano na wengine. Ili mwanaume amteke kimapenzi mwanamke lazima awe nyuma yake hata kama atakuwa na kosa. Wanawake wengi hupenda kuelimishwa zaidi kuliko kufokewa. Kuwa chaguo namba moja Safari ya penzi la mwanamke haishii kwenye kumpata na kumliki, kisha kujisahau kwa kisingizio kuwa umemuoa au umemvisha pete ya uchumba, ni zaidi ya hapo. Jambo la tatu ambalo wanawake wengi huhitaji ni kuwa namba moja au kupendwa. Wanapenda watangulizwe katika mapenzi ...

Mambo 10 ukiyazingatia wewe ni mke bora katika ndoa

Image
UHALISI WA MAISHA: Maisha halisi ya mwanamke anayetarajia kuwa mke/ mke tayari hii ni kumaanisha kuwa wanawake mashujaa tunapaswa kuishi maisha ambayo yanatutambulisha kama mfano wa kuigwa ili tunapozungumza na kufundisha mabadiliko tuwe tunazungumza uhalisia wa maisha yetu ambao unajengwa na haya yafuatayo; UVUMILIVU: Kuwa mvumilivu katika maisha yake ya kila siku hasa ukizingatia kuwa tunakutana na mambo mbali mbali yasiyotuvutia katika mahusiano yetu, mengine ni magumu na yanayokwenda kinyume kabisa na matakwa yetu au mazoea yetu ya binafsi. Ifahamike kwamba wewe kama mwanamke shujaa inapotokea umekutana na mambo kama haya hupaswi kuonyesha hasira zako wazi wazi kama vile; chuki, kulaumu, ugomvi, vurugu, malalamiko, manung’uniko, machafuko, kulipa kisasi au aina yoyote ya uharibifu kutokea kwako au ndani mwako. Hivyo mwanamke shujaa huwa ni heri kila anapokuwa kwani hutunza amani ya eneo alipo. UPENDO WA DHATI: Maisha ya upendo wa halisi na sio wa kinafki kwa jamii inayomz...

Sababu 20 Kubwa Ambazo Zinakufanya wewe Mwanaume Usipate Mpenzi

Image
Tangu ujielewe umekuwa single. Huna girl friend ama mpenzi yeyote yule. Kuna yule mwanamke jirani yako kila siku unamwona. Unamtamani lakini hutaki kumuapproach. Kiufupi unaishi kiupweke ilhali marafiki zako kila wakati wanaonekana na wanawake tofauti tofauti. Hii ni hali ambayo inatokea kwa wanaume wengi duniani. Usijione kama ni wewe pekeako. So shida huwa inatokea wapi? Nesi Mapenzi tumekuja na sababu ambazo zinakufanya wewe ubaki single milele. #1 Hautaki kujaribu. Kuna wanaume wengi ambao wanalalamika kuwa hawana wachumba lakini hapo hapo hawatii bidii kuhakikisha kuwa wanatafuta mmoja. Usipojaribu kutongoza mwanamke basi utabaki hivyo hivyo single milele. #2 Unatafuta mwanamke aliyekamilika. Wanaume wengine hufanya kosa la kutafuta wanawake warembo zaidi katika hii dunia. Hili ni jambo ambalo hutalipata. Kama utasema hutafuti mwanamke mpaka awe anafanana na Masogange ama Huddah Monroe basi utangojea sana. #3 Hauko huru. Si jambo baya kuishi na wazazi wako. Wanaume wengi bad...

Kama wewe ni mwanamke jihadhari na hizi Tabia kwa mumeo

Image
1. CHOKOCHOKO Wanaume wengi huwa hawapendi chokochoko. Hawapendi mwanamke ambaye yeye kila wakati ni kuanzisha chokochoko ambazo zinazalisha ugomvi. Wanaume wengi hawapendi mabishano. Hawapendi ugomvi hivyo mwanamke anapokuwa hodari wa kuleta chokochoko, huepukwa. Ni vyema basi mwanamke akachunga kauli. Akawa si mtu wa kuchimbachimba vitu ambavyo havina kichwa wala miguu. Asiwe na kisirani. Kinywa chake kitawaliwe na maneno matamu, yatakayomtia moyo mpenzi wake, yatakayomfariji na yatakayomfanya apende kuzungumza naye. Mara nyingi mwanaume akiona mke au mpenziwe ni mtu wa kupenda chokochoko, mara nyingi humuepuka. Anajitahidi kadiri ya uwezo wake kukaa naye mbali. Ataona ni bora achelewe kurudi nyumbani akakutane na marafiki baa, wapige stori ili muda uende na akirudi nyumbani asiwe na muda wa kuzungumza na mwenzi wake, yeye ni kula na kulala. 2. KUTORIDHIKA Wanaume wengi wanachukia kuwa na wanawake wasioridhika. Baadhi ya wanawake hata uwape nini huwa hawaridhiki. Wanawasumbua...

Wamepanda Bei Sana Siku Hizi…

Image
Waume za watu bwana siku hizi watamu kama wametiwa sukari ya dubai! Ukiwaonja hunasuki! Yaani kama sumu isivolambwa. Haramu lakini tamu! Na hii inatoakana na Mabachelor kuchushaaa! Sifa kuu za waume za watu wengi ni hizi (Yaani mambo yao kama universal vile! utazani kuna standardiztion ilifanyika) 1. Wanahonga Balaaaaaaa! Kwa wale wasitaarabu mtaita wanajali! Yaani wanajua kujikombaga mweeeeee! Wala huna shida ya kumkumbushia shida yako! Mwenyewe tu anakujali. Akiona huna usafiri atakujali hata kwa tax, pesa ni kiunganishi, kodi atatoa tu wala si mbishi. Ndo maana ma Miss Tz wengi wamefanya mapinduzi ama wamejiweka kwa waume za wenzao. 2. Wamepevuka kiakili na wanajua kumhandle mwanamke. After yrs of constant nagging and endless bettles na wifey lazima akili zimkae fresh. Yaani the wife did all the coaching, so ukimpa weye anajua what he better does or else……! Sio mabachelor manshindana kama mtu na mke mwenzie. Chezea kujikuta situation ya No Way Out all you can do is make up wit...

MAPENZI: DALILI ZA AJABU ZA MWANAUME KUWA NI SHOGA….

Image
Siku hizi wanaume wengi wamekuwa na tabia mbaya za ushoga ..wengine wanaonyesha live wengine wanajificha ficha ila kuna dalili unaweza kujua kuwa ana tabia hizi ,,,Hizi ni Baadhi tu ukiona mvulana ana tabia hizi basi anza kumchunguza vizuri inawezekana kabisa kuwa si ridhiki… 1. Kutia kalikiti kichwani 2. Kujichubua 3. Kutinda nyusi/kujiangalia sana kwenye kioo 4. Kutoboa pua/sikio 5. Kupaka lip shine 6. Kuvaa nguo za kuacha mattako nje 7.Umbea 8.Kupigana vijembe 9.Kupenda taarabu 10. Kurembua macho/Kulegeza sauti 11.Endeleza

Tabia Nne za Mpenzi Asiyekuwa na Penzi la Kweli.

Image
Ifahamikekuwa hakuna asiyehitaji mapenzi ya kweli ingawa kuna wapenzi wanaothamini penzi wmenzi wake anapokuwa na pesa au kazi Fulani na baada ya hapo hujitoa katika mahusiano hayo hali ambayo huleta kwikwi katika mtima wa moyo wa anayefahamu kupenda. 1.      Muongo Hakuna asiyefahamu athari za mtu muongo katika jamii, vivyo hivyo ndivyo ilivyo katika mapenzi uongo ni sumu mbaya na nidalili moja wapo ya kuonyesha kuwa mpenzi wako hana penzi la dhati nawe na huyo aweza kukuletea athari za kufikiri hapo baadae endapo hautakuwa makini nae. Hivi karibuni nilikuwa mjini Mbeya nikipata chakula katika moja ya mgahawa uliopo mkabala na Posta, katika mgahawa huo nilikutana na vijana wawili na msichana mmoja wakiwa wanakula chakula ambapo kati ya kijana mmoja alionekana kuwa ni mpenzi mpya wa yule binti ambaye alisikika akisema kiwa ‘’ukija kwangu atakalia sofa ambazo hujawahi kuziona maishani’’ hali iliyonishtua na kuelewa mara moja kati ya tabia alizonazo kijana yule ambay...