Barnaba ammwagia sifa Dogo Aslay

Kupitia kipindi cha eNewz cha EATV Barnaba alisema anafurahishwa na jinsi nyimbo za Aslay zinavyopendwa na kupenya sana uswahilini bila msanii huyo kutumia nguvu kubwa ya kiki au 'interview' nyingi.
"Aslay yupo sawa kabisa, kitu kizuri ni kwamba mashabiki wanaongea wenyewe, uswahilini nyimbo zake zinapendwana sana na kwa sasa yeye ndiye msanii anayefanya vizuri kwa upande wangu" - Barnaba Classic
Aidha Barnaba alisema Aslay anaandika stori nzuri sana huku akiwakumbusha wasanii wakubwa kuangalia anachokifanya msanii huyo na kujifunza.
"Napenda sana anachokifanya Aslay, kwanza anaandika stori nzuri sana, mfano wimbo wake 'Mhudumu', au 'Danga' hata 'Ndoa" aliyomshirikisha Khadija Kopa" aliongeza msanii huyo.
Aslay alikuwa mmoja wa wasanii waliounda kundi la Yamoto Band ambapo kwa sasa anafanya kazi zake mwenyewe, tangu aanze kufanya kazi nje ya kundi Aslay ameshaachia nyimbo kama 'Angekuona', 'Usiitie Doa', 'Mhudumu', 'Baby' n.k

Comments


Popular posts from this blog

ILE SINTOFAHAMU YA NANI BINGWA WA VPL HII HAPA

Michezo:Ajibu huyo yanga

ELIZABETH MICHAEL ' LULU' awafungukia wasanii wa bongo move

fahamu kilichojiri nyumbani kwa Tundulisu