mimi nipo sex Lulu diva



Muimbaji Lulu amekiambia kipindi cha Uhondo cha E Fm kuwa alitambua kuwa yeye ni mzuri kutokana na sifa alizokuwa akipewa na mama yake mzazi kitu ambacho kilimfanya kutolaghaika na watu waliokuwa wakimsifia.
“Mimi ni msichana ambaye nipo sex ambaye nina mvuto, mama yangu alikuwa akiniambia Lulu mwanangu mashallah, yaani hapa sidhani kama kuna mtu nitamwambia idadi ya ng’ombe ninazozitaka halafu akapindua,” amesema na kuongeza.
“Na mimi mwenyewe nikawa najiona ndio maana hata sikuweza kurubunika, yaani ile mtu kuniambia wewe mzuri akanidanganya kwa vichipsi mayai, mwenyewe nilishajijua ni mzuri,” amesema Lulu Diva.
Hitmaker huyo wa Usimwache kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake inayokwenda kwa jina la Utamu.

Comments


Popular posts from this blog

Tabia Nne za Mpenzi Asiyekuwa na Penzi la Kweli.

Wsanii wanaowania MTV Europe Music Awards

KUTOKA IKULU:Rais Magufuli amefanya uteuzi mwingine leo julai 6 2017

messi aamua kutokuwa mbinafsi

Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu mikononi mwa polisi