Wabunge Uganda wataka kuondoa ukomo wa urais

Wabunge wa Chama tawala Nchini Uganda cha National Resistance Movement (NRM) cha Rais wa sasa wa nchi hiyo, Yoweri Museveni wamekubaliana kuwasilisha bungeni mswada wa kuondoa ukomo wa umri wa rais kutoka kwenye katiba ya nchi hiyo.
Katiba ya Uganda kwa sasa hairuhusu mtu yeyote mwenye umri zaidi ya miaka 75 kugombea nafasi ya urais wa nchi hiyo ili kutoa wigo kwa vijana ambao bado wana nguvu za kuweza kulitumikia taifa lao.
Aidha, Rais wa sasa wa nchi hiyo, Yoweri Museveni ana umri wa miaka 73, ambapo ni miongoni mwa viongozi waliotawala kwa muda mrefu zaidi barani Afrika na amekuwa madarakani kwa zaidi ya miongo mitatu.
Hata hivyo, Uchaguzi Mkuu wa Urais nchini humo unatarajiwa kufanyika mwaka wa 2021 ambapo rais wa sasa atakuwa ameshavuka miaka kadhaa umri huo.

  Na dar24

Comments


Popular posts from this blog

Afariki kwakuchomwa na kisu

SUGU;:Tundu lissu ameniagiza niwaambie haya

VPL; Ngoma ngumu

STAR "ZARI THE BOSS LADY" APEWA USHAURI HUU

Messi amuandikia Neymar ujumbe huu.

Picha 10:madaraja makubwa na bora duniani

Jaji Mutungi ayatolea nje maamuzi ya CUF ya Maalim Seif

mimi nipo sex Lulu diva