Mwandishi wa Mwananchi Tumaini Msowoya na Mkuu wa Kituo cha Nyota ya Asubuhi, Sister Idda Luizer wakiwa na mapacha, Maria na Consolata By Tumaini Msowoya, Mwananchi tmsowoya@mwananchi.co.tz Jana tuliishia sehemu inayoeleza jinsi pacha hawa walioungana, Maria na Consolata, wanavyochangia hisia za baadhi ya viungo vyao. Pengine ni kuchangia huko kwa hisia za viungo, kumefanya wawe pia na hisia moja katika masuala ya kimaisha. Wawili hawa wanahisia moja ya kimapenzi. Sasa endelea… Si rahisi kufikiria maisha ya ndoa ya Maria na Consolata kwa jinsi walivyo, lakini pacha hawa walioungana wako wazi kuhusu matamanio yao ya maisha ya ndoa. Katika mazungumzo yao na gazeti hili, Maria na Consolata waliweka bayana mipango yao ya ndoa mara watakapomaliza elimu ya chuo kikuu. Ingawa ni kitu cha kushangaza, Maria na Consolata hawatakuwa mapacha wa kwanza katika maisha ya ndoa. Chang na Eng Bunker ni pacha wanaume waliozaliwa mwaka 1811 nchini Thailand ambako zamani kuliitwa Siame. ...
Comments