Kenyata sina matakwa yoyote kutoka IEBC

Katika majadiliano hayo Rais Uhuru amesema yuko tayari kwa uchaguzi na hana matakwa yoyote kutoka IEBC, zaidi ya chombo hicho kutekeleza wajibu wake wa kusimamia uchaguzi mpya wa raia Oktoba 26 kama ulivyoamriwa na Mahakama ya Juu.
Kikao hicho kilifanyika katika Jengo la Harambee, ambako imo ofisi ya Rais katikati ya jiji na kilihudhuriwa pia na Makamu wa Rais William Ruto.
“Tuliweka wazi kwamba hatuna matakwa au masharti kuhusu suala hili. Tumetenga fedha kwa ajili ya IEBC kufanya kazi yake. Sasa watekeleze wajibu wao,” alisema Rais.
“Tunasisitiza kwamba uchaguzi ufanyike Oktoba 26, muda uliopangwa na IEBC kama masharti baada ya uchaguzi wa Agosti 8 kufutwa,” aliongeza.
Septemba Mosi, Mahakama ya Juu ilifuta matokeo ya urais ya Agosti 8 ikidai ilijiridhisha kwamba ulijaa dosari na kukosa uhalali. Tangu wakati huo Rais na makamu wake wamefanya kampeni nzito katika kaunti zote kwa ajili ya uchaguzi huo wa marudio.
  

Comments


Popular posts from this blog

Afariki kwakuchomwa na kisu

Prof. Maghembe atoa neno kwa wavamizi wa misitu.

mimi nipo sex Lulu diva

Wabunge wanamna hii kufukuza ccm

Maajabu ya pacha walioungana, wajikuta katika penzi moja .

Mtanzania aliyekataa mshahara wa Tsh. milioni 425 Marekani amerejea nyumbani

Barcelona sasa yawa moto baada ya hili

Mwanamke yeyote nampenda, awe mweusi, mweupe, mwembamba au unene – Timbulo

Mtandao wa biashara ya ngono wavunjwa