Prof. Maghembe atoa neno kwa wavamizi wa misitu.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe amewashukuru wavamizi wa Msitu wa Hifadhi wa Isawima wilayani Kaliua ambao wameamua kwa hiari yao kubomoa makazi na kuondoka wao na mifugo yao katika eneo hilo ambalo ni miongoni mwa vyanzo vya maji ya Ziwa Tanganyika .
Ameyasema hayo Wilayani Kaliua mara baada ya kusomewa taarifa ya utekelezaji wa zoezi la kuwaondoa Wavamizi hao katika Msitu wa Hifadhi na kutembelea eneo walipoondolewa wavamizi na kisha kupata fursa ya kuongea na wananchi.
Amesema kuwa Serikali imefurahishwa na uamuzi huo uliochukuliwa na watu hao baada ya kupata elimu kuhusu athari za kimazingira za wao kung’ang’ania kuendelea kuishi katika maeneo yaliyohifadhiwa na kuamua kuondoka bila kushurutishwa.
“Serikali haina shida ya kumuonea mtu na ndio maana tumekuwa tukiitumia zaidi elimu jambo ambalo limeleta mafaniko makubwa katika eneo la Hifadhi hii ambapo zaidi ya asilimia ya 70 ya watu waliokuwa wamevamia wameondoka,”amesema Prof. Maghembe

Comments


Popular posts from this blog

Afariki kwakuchomwa na kisu

Wabunge wanamna hii kufukuza ccm

Maajabu ya pacha walioungana, wajikuta katika penzi moja .

Mtanzania aliyekataa mshahara wa Tsh. milioni 425 Marekani amerejea nyumbani

Barcelona sasa yawa moto baada ya hili

Mwanamke yeyote nampenda, awe mweusi, mweupe, mwembamba au unene – Timbulo

Mwezi Mtukufu… Roma Awafuturisha Watoto Yatima

BREAKING NEWS, TANGA polisi watumia mabomu kutawanya watu

Mbunge wa kigoma atafaute kazi nyingine