WATUMISHI 400 WENYE ELIMU YA DARASA LA SABA SERIKALINI KUFUKUZWA KAZI


Zaidi ya Wafanyakazi 400 wa Serikali wanatarajia kuondolewa kazini mkoani Morogoro kutokana na kushindwa kujienmini deleza kielimu baada ya kuajiriwa miaka 13 iliyopita wakiwa na vyeti vya elimu ya msingi.
Watumishi hao ambao wengi wao ni wauguzi, wahudumu wa afya, madereva, wahudumu wa ofisi, watendaji wa mitaa, vijiji na kata tayari wamenyimwa mishahara yao ya mwezi huu.
Akizungumzia zoezi hilo aliyekuwa Mtendaji wa Kata ya Kimamba wilayani Kilosa, Mashaka Motile amesema katika wilaya hiyo watumishi zaidi ya 80 wamenyimwa mshahara bila maelezo yoyote na walipofuatilia ndipo walipofahamishwa kuwa walipewa muda wa kujiendeleza na wameshindwa kufanya hivyo.
“ amesema.
Motile anasema yeye na baadhi ya watendaji wengine walisimamishwa kazi kimakosa kwani agizo linasema wasimamishwe kazi walioajiriwa kuanzia Mei 20, 2004 lakini wao waliajiriwa Mei Mosi, 2004.
Akizungumzia uamuzi huo wa Serikali, mhudumu wa afya wa manispaa ya Morogoro ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema uamuzi huo umekuwa wa ghafla mno na haujatoa muda wa wao kujiendeleza.
amesema.
Alipotakiwa kuzungumzia zoezi hilo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Kilosa, Kessy Mkambala alisema bado zoezi linaendelea litakapokamilika ndo ataweza kulizungumzia.
Naye Katibu wa Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) mkoani Morogoro, Lawrence Mdega amesema wamepokea malalamiko toka kwa wafanyakazi zaidi ya 150 wanaolalamika kuondolewa kwa kuwa wana elimu ya msingi.
“Nimeshawasilisha haya malalamiko makao makuu ya TALGWU ili washughulikie lakini tunachotaka watumishi hawa walipwe mshahara wa Julai ambao tayari waliufanyia kazi lakini pia walipwe mafao yao maana waliitumikia Serikali kwa uadilifu na vyeti vyao hivyo vya elimu ya msingi.
Na MtaaKwaMtaa

Comments


Popular posts from this blog

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAPILI 27.08.2017

Maajabu ya pacha walioungana, wajikuta katika penzi moja .

Picha sita 6 mende wamaajabu duniani

TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMISI 31.08.2017

TANZIA: Aliyewahi kuwa mbunge wa Moshi Mjini, Mzee Philemon Ndesamburo(CHADEMA) aaga dunia

Picha ya Beckham na mtoto wake Serengeti imeleta mjadala hadi kwao

MTWARA:watu watano wanashikiliwa na Jeshi la polisi

MANARA AMKABIDHI JPM KIWANDA

Jux afunguka haya kuhusu vanessa mdee

Marekani yatishia vikwazo kwa yeyote atakaekwamisha uchaguzi DRC