Neymar mbioni kutua Psg

Mshambuliaji wa Barcelona Neymar, 25, amekubali kusaini mkataba wa miaka mitano kujiunga na Paris Saint-Germain na huenda akakamilisha uhamisho wa pauni milioni 197 wiki ijayo. (RMC)
PSG watawapa Barcelona Angel Di Maria, 29, kama sehemu ya mkataba wa kumsajili Neymar, ili kupunguza kodi ya kutengua kifungu cha uhamisho cha mchezaji huyo wa Brazil. (AS)
Iwapo Neymar ataondoka, Barcelona wataamua kuwawinda wachezaji watatu kutoka EPL- Philippe Coutinho, 25, wa Liverpool, Eden Hazard, 26, wa Chelsea, na Delle Alli, 21 wa Tottenham kuziba pengo. (Mirror)
Barcelona wana wasiwasi kuwa bei kubwa ya kumsajili Philippe Coitinho kutoka Liverpool huenda ikawakatisha tamaa. (AS)
Kiungo wa Barcelona Andres Inisesta, 33, amesema ni Neymar pekee anayeweza kuzungumzia kuhusu hatma yake, akisema hadhani kama euro milioni 200-300 zina manufaa yoyote kwa klabu bila Neymar mwenyewe. (Marca)
Monaco wanasisitiza kuwa hawatamuuza Thomas Lemar, 21, licha ya Arsenal kupanda dau la tatu la takriban pauni milioni 45 kumtaka kiungo huyo.

Comments


Popular posts from this blog

ILE SINTOFAHAMU YA NANI BINGWA WA VPL HII HAPA

Michezo:Ajibu huyo yanga

ELIZABETH MICHAEL ' LULU' awafungukia wasanii wa bongo move

fahamu kilichojiri nyumbani kwa Tundulisu