SABABU YA KUWAKAMATA WAFANYAKAZI WA ACACIA HII HAPA

Idara ya Uhamiaji   imesema jukumu la Udhibiti wa Uingiaji na Utokaji wa raia wa kigeni nchini, linatekelezwa kwa mujibu wa Sheria ya Uhamiaji Sura ya 54 (Rejeo la 2016) na wala haiwalengi wafanyakazi wa Kampuni ya Madini ya Acacia peke yake.
Ni hitajio la kisheria kwa kila raia wa kigeni anayeingia na kutoka nchini kukaguliwa ili kujiridhisha iwapo hakuna dosari zozote za Uhamiaji, Ulinzi na Usalama.
Sheria ya Uhamiaji inaitaka Idara ya Uhamiaji kumhoji mtu yeyote awe raia wa Tanzania au kigeni bila kujali anafanya kazi kwenye Kampuni au Shirika gani, pale inapotaka kujiridhisha juu ya uhalali wa ukaazi wake hapa nchini na ikijiridhisha kuwa mtu huyu hana dosari zozote inamwachia huru kama ilivyofanyika kwa wafanyakazi wa Kampuni ya Madini ya Acacia waliohojiwa na kuruhusiwa kuendelea na safari yao hivi karibuni.
Idara ya Uhamiaji inapenda kuuarifu Umma kuwa hakuna sababu zozote nje ya matakwa ya Sheria  ya Uhamiaji zinazopelekea Idara ya Uhamiaji kuweka kizuizi  cha kuja au kutoka kwa wafanyakazi wa kigeni wa Acacia.
Tunapenda kuujulisha Umma kuwa ni muhimu kwa watanzania na raia wa kigeni wanaokusudia kuingia na kutoka nchini kuhakikisha wanafuata Sheria za Uhamiaji ili kutimiza hitajio la kisheria.

Comments


Popular posts from this blog

wawili wamefariki dunia katika majibizano ya risasi

Jumuiya ya Freemasons imetoa tahadhari nzito kwa Watanzania

Taarifa ya Serikali baada ya kauli za jana za Tundu Lissu

waziri mkuu majaliwa awa mkali

Kilichomkorofisha Mke wa Roma

. Ridhiwani Kikwete amefunguka haya kwa wananchi na baadhi ya viongozi wakae

Spika Ndugai Aagiza Kubenea Kusakwa, Zitto Kufikishwa Kwenye Kamati ya Maadili

Msigwa tunawindwa wabunge wanne CHADEMA -