Mahanga akamatwa na Polisi

Dar es Salaam. Mbunge wa zamani wa Ukonga na Segerea, Dk Makongoro Mahanga amekamatwa na Polisi Mkoa wa Ilala kwa amri ya Mahakama Kuu na amefikishwa mahakamani.
Mahakama iliamuru Dk Mahanga akamatwe na kufikishwa mahakamani kwa kushindwa kutekeleza uamuzi unaomtaka amlipe mdai Kainerugaba Msemakweli Sh14 milioni.
Fedha hizo ni gharama za kesi alizozitumia Msemakweli baada ya kushinda kesi ya madai ya kashfa ambayo Dk Mahanga alimfungulia kwa kumtaja kwenye kitabu chake kinachoitwa: “Mafisadi wa Elimu”.
Katika kitabu hicho anamtaja kuwa ni mmoja wa viongozi wenye shahada za udaktari wa kughushi.
Kati ya kiwango hicho cha fedha, Dk Mahanga ameshalipa Sh6 milioni hivyo anadaiwa Sh8 milioni.
 Na mwananchi

Comments


Popular posts from this blog

wananchi wamshtaki polisi kwakuwanyanyasa

sharti la polepole lapata upinzani

KENYA:Tume Huru ya Uchaguzi yaridhia maombi ya upinzani

Angelina Jolie kuonekana kwenye jarida la ‘Vanity Fair’.

Afisa wa serikali ajinyonga

Viongozi wa G7 waangazia bara la Afrika

UEFA kuendelea kutimuavumbi hii leo

YANGA YASHUSHA STRAIKA WA AFCON