, Tundu Lissu akiwa sambamba na Dkt. HEllen Kijo-Bisimba



Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Tundu Lissu akiwa sambamba na Dkt. HEllen Kijo-Bisimba ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na baadhi ya mawakili wanaounga mkono wito uliotolewa na Tundu Lissu wa kuwataka mawakili wote kugomea kufika Mahakamani kutekeleza majukumu yao ya kisheria ikiwa ni kuonyesha msimamo wao wa kupinga kitendo cha jengo la mawakili wa IMMA kulipuliwa kwa kile kinachodhaniwa kuwa ni bomu la petroli.

Hata hivyo, wito huo haukuitikiwa na mawakili wengi kama ilivyotarajiwa na Tundu Lissu kwani wengi walifika kusikiliza kesi zinazowahusu katika mahakama mbalimbali nchini.

"Sio kwamba sisi hatujaguswa na kilichowapata wenzetu wa IMMA Advocates isipokuwa hili la Rais wao Tundu Lissu ni kuchanganya mambo mawili yasiyohusiana kwani kuchomwa kwa ofisi tayari Polisi wanafanya uchunguzi na hawajatoa majibu na hiyo ni Taasisi iliyo chini ya Serikali ambapo Mahakama ni mhimili unaojitegemea hauingiliani kimajukumu na Serikali. Sasa kuchanganya hizi Taasisi mbili sio sahihi kabisa!" waisema baadhi ya mawakili walioendelea na majukumu yao hapo jana.

Aidha mawakili hao walisema "sisi Mahakamani tunawawakilisha wateja wetu ambao ndio waliotuajiri ili tuwawakilishe kwenye kesi zao. Tuna mikataba yao kisheria na hilo Tundu Lissu analifahamu na kisheria kugomea kutekeleza majukumu ya kimkataba kwa suala lililo nje ya mkataba husika ni kosa linaloweza kutufanya kushitakiwana wateja wetu."

Comments


Popular posts from this blog

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAPILI 27.08.2017

Maajabu ya pacha walioungana, wajikuta katika penzi moja .

Picha sita 6 mende wamaajabu duniani

TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMISI 31.08.2017

TANZIA: Aliyewahi kuwa mbunge wa Moshi Mjini, Mzee Philemon Ndesamburo(CHADEMA) aaga dunia

Picha ya Beckham na mtoto wake Serengeti imeleta mjadala hadi kwao

MTWARA:watu watano wanashikiliwa na Jeshi la polisi

MANARA AMKABIDHI JPM KIWANDA

Jux afunguka haya kuhusu vanessa mdee

Marekani yatishia vikwazo kwa yeyote atakaekwamisha uchaguzi DRC