TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAPILI 27.08.2017


Liverpool wameweka makataa ya hadi Jumatatu, kwa Barcelona wawe wamefikia bei ya Philippe Coutinho, 25. (Onda Cero)

Liverpool wanataka kukamilisha usajili wa  Alex Oxlade Chamberlain, 24, kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Chelsea pia wanamtaka winga huyo wa Arsenal. (Sunday Mirror)

Mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28, imeripotiwa anaitaka klabu yake kumfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika EPL iwapo wanataka asaini mkataba mpya. (Daily Star)

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger hajakata tamaa ya kumsajili Thomas Lemar wa Monaco, 22,  pamoja na Virgil van Dijk, 26, ingawa huenda ikawa msimu ujao. (Sun)

Arsenal wanataka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Marco Asensio, 21. (Sunday Express)

Paris Saint-Germain wanaendelea na majadiliano ya kumsajili mshambuliaji wa Monaco Kylian Mbappe kwa pauni milioni 166 kabla ya dirisha la usajili kufungwa, ingawa Monaco wenyewe wanataka Mbappe aende Real Madrid. (Sunday Telegraph)

Iwapo Kylian Mbappe ataondoka Monaco, klabu hiyo itataka kuziba pengo lake na Islam Slimani, 29, wa Leicester City. (Leicester Mercury)

Kiungo wa Bayern Munich Renato Sanchez, 20, ameomba kuachwa kwenye kikosi dhidi ya Werder Bremen ili ashughulikie mustakbali wake huku Chelsea na Liverpool zikimfuatilia. (Metro)

Everton wanataka kuwapiku Chelsea katika kumsajili mshambuliaji wa Leicester Jamie Vardy, kwa pauni milioni 40. (Sunday Mirror)

Tottenham huenda wakataka kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Divock Origi, 22, iwapo Vincent Janssen ataondoka. (Sun)

Juventus wanataka kumsajili kiungo wa Barcelona Andre Gomes, 24. (Marca)

Mmiliki wa Valencia amewasili mjini Manchester kuanza mazungumzo ya kumsajili kiungo wa Manchester United Andreas Pereira, 21. (Sunday Express)

Leicester City wanataka kumsajili beki wa Manchester United Chris Smalling. (Daily Mirror)

Beki wa PSG Serge Aurier anasubiri kibali cha kufanya kazi Uingereza baada ya kukamilisha vipimo vya afya ili kujiunga na Tottenham. (Sky Sports)

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Jumapili njema.


  Na salim

Comments


Popular posts from this blog

Uchumi wa taifa la Korea Kaskazini waimarika

harakati za ndesamburo na utajiri wake hizihapa

ACACIA wapinga vikali matokeo ya kamati ya pili ya Rais

IsraelIsrael yasalimu

mimi nipo sex Lulu diva

Real madrid mabingwa tena UEFA

Rais Zuma akiri kunusurika kuuawa kwa sumu

Hatua 10 Muhimi za Kumchagua Mchumba Mtakae Funga Ndo. a tzaama SOMA NA SHARE HII

Watu kumi na mmoja wauawa katika shambulio