Mgogoro mwingine Chadema na serikali

Katika kikao alichofanya na wanahabari, Mwenyekiti wa CHADEMA, Halmashauri ya mji wa Tunduma, Ali Mwafongo ameleezea kusikitishwa na amri hiyo ya mkuu wa wilaya na kusema kuwa kamwe hawatarudi nyuma huku akiahidi kutompa ushirikiano mkuu wa wilaya huyo.
“Uchungu tunaopata sasa hivi tunajua ipo siku itakuwa furaha kwetu kwani ushindi unakaribia. Kinachofanywa sasa hivi wakumbuke ipo siku watawala watakuwa wapinzani na haya yanayofanywa hayataweza kuturudisha sisi nyuma. Viongozi wetu wamekuwa wakipelekeshwa sana lakini katu hatutokata tamaa kwa sababu ni kazi yetu kusema ukweli na kuwatumikia wananchi wetu ” alisema
Mbali na hayo mkuu huyo wa wilaya pia ametuhumiwa kutoa amri ya kushusha bendera za chama hicho hali ambayo imeonesha kuwakera baadhi ya viongozi wakiwemo madiwani.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo, Juma Irando amekiri kutoa amri ya kukamatwa kwa mbunge huyo kwa madai kuwa ametoa kauli ya kudharau mamlaka ya uteuzi.
Mbunge Mwakajoka amekamatwa Jumanne na kuwekwa ndani ikiwa ni siku moja tu baada ya Mbunge mwingine wa Jimbo la Vwawa, Paschal Haonga kukamatwa na jeshi la polisi.

Na mtembezi.com

Comments


Popular posts from this blog

ILE SINTOFAHAMU YA NANI BINGWA WA VPL HII HAPA

Michezo:Ajibu huyo yanga

ELIZABETH MICHAEL ' LULU' awafungukia wasanii wa bongo move

fahamu kilichojiri nyumbani kwa Tundulisu