Wakitoa malalamiko hayo kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mh. Christina Mndeme ambaye kwa mara ya kwanza amefanya ziara ya kikazi wilayani Tunduru tangu kuteuliwa kwake Octoba kushika wadhifa huo, baadhi ya wananchi hao wa Tunduru wamesema askari huyo amekuwa akiwanyanyasa kwa kuwabambikiza kesi na wakati mwingine kukamata wananchi wakiwa kwenye shughuli za uzalishaji mali akiwaita wazururaji. Akijibu malalamiko hayo ya wananchi, Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Tunduru, Mrakibu Mwandamizi wa jeshi la Polisi, Mwakasanda amesema ameshaagiza askari Polisi huyo akamatwe popote alipo na kuwekwa ndani kwa uchunguzi zaidi. Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mh, Christina Mndeme amewaonya askari polisi kuacha tabia ya kubambikizia kesi wananchi na badala yake watende haki huku akiwataka wananchi wasiogope kutoa taarifa polisi endapo wanafanyiwa vitendo hivyo ili hatua zaidi zichukuliwe.
Wakati katibu wa oganaizesheni wa CCM, Pereira Silima akikanusha kupitishwa kwa sharti la ukazi kwa wagombea udiwani na ubunge, chama hicho kimewataka watumishi wa umma walioshinda uchaguzi katika ngazi ya wilaya kuamua moja; ajira au siasa. Juzi, katibu wa uenezi wa CCM, Humphrey Polepole alisema katika kipindi cha redio cha Times FM kuwa wanaogombea udiwani na ubunge mwaka 2020 watatakiwa kuwa wakazi wa maeneo wanayogombea, lakini mara moja akapata maswali kutoka kwa wanachama. Lakini jana, Silima alisema CCM haiwezi kuweka sharti hilo kwa kuwa linakiuka Ibara ya 67 (1 a-c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ambayo inaeleza sifa za mtu ambaye hatakuwa na sifa za kugombea, hali kadhalika Sheria za Uchaguzi. “Nikiwa katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa mwenye dhamana ya uchaguzi, napenda kuwajulisha kwamba Chama cha Mapinduzi kimefanya mabadiliko katika katiba yake,” anasema Silima. “Mabadiliko ambayo yamepitishwa na Mkutano Mkuu wa CCM Taifa uliofanyika 12/03/2017, pamoja na kanuni...
Nairobi, Kenya. Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Wafula Chebukati ametangaza timu ya maofisa watakaosimamia shughuli za uchaguzi wa marudio Oktoba 26 huku jina la ofisa mtendaji mkuu, Ezra Chiloba likikosekana. Chebukati, wakati anatangaza majukumu ya maofisa hao Ijumaa alisema Chiloba, ambaye muungano wa National Super Alliance (Nasa) unataka aondolewe, hatakuwa na mkono katika uchaguzi huo. Mbali ya Chiloba, pia maofisa wengine saba hawamo. Hatua hiyo imekuja muda mfupi baada ya maandamano makubwa kufanywa na wafuasi wa Nasa mjini Kisumu, Nairobi na Homabay wakishinikiza kuondolewa na Chiloba na wenzake 10. Vilevile, mabadiliko hayo yamefanyika wakati Nasa wakitangaza kuongeza siku ya Jumatano katika siku za maandamano. Katika barua yao waliyopeleka polisi sasa Nasa watakuwa wakiandamana kila Jumatatu, Jumatano na Ijumaa kushinikiza maofisa 11 waondolewe, na zifutwe zabuni kwa kampuni ya kuchapisha makaratasi ya kupigia kura na inayosambaza vifaa vya utambu...
Muigizaji wa filamu Hollywood Marekani, Angelina Jolie anatarajiwa kukava jarida la ‘Vanity Fair’ linalotoka Septemba 2017.Katika jarida hilo Angelina atazungumzia maisha yake ya sasa pamaoja na mahusiano aliyokuwa nayo na aliyekuwa mumewe Brad Pitt. Picha zitakazokuwa katika jarida hilo. Mahusiano ya mwanamama huyo na Brad Pitt waliisha mna mwaka jana baada ya kuvunja ndoa yao waliofunga mwaka 2014 na walibahatika kupata watoto sita kati yao wapo awalioawasili.
Kamboi ambaye alikuwa anafanya kazi katika Idara ya Afya kama Afisa Ugavi, aliacha ujumbe akieleza kuwa amepata msongo wa mawazo baada ya kutolewa amri na Gavana wa jimbo hilo, kuchunguzwa iwapo amehusika na vitendo vya uhujumu uchumi, huku akiwataja maafisa wenzake ndiyo waliostahili kubeba msalaba huo. Kamanda wa Polisi wa jimbo la Nandi nchini Kenya, Peter Wambani amesema marehemu alimuomba mke wake akamuandalie kikombe cha chai huku akiendelea kutazama mpira sebuleni, lakini aliporudi hakumkuta mumewe na baada ya kumtafuta alikuta mwili wake ukining'inia kwenye mti karibu na banda la ng'ombe. Tukio hilo limetokea huku baadhi ya maafisa wengine wa idara hiyo wamesimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi, kutokana na kupotea kwa fedha za serikali. Na eatv
Viongozi kadha wa nchi za Afrika wanahudhuria siku ya pili ya mazungumzo katika mkutano huo wa G7, ili kujadili tatizo la wahamiaji. Itali iliamua kuandaa mkutano huo huko Sicily, ili kuvutia macho ya ulimwengu juu ya shida za Waafrika wanaohatarisha maisha yao, kuvuka Mediterranean ili kuingia Ulaya. Tayari mwaka huu, wahamiaji elfu hamsini wameingia Italia, huku 1500 wamezama safarini. Kwa hivyo viongozi wa G7 wamezungumza na wenzao kutoka Tunisia, Kenya, Ethiopia, Niger na Nigeria, kutafuta njia za kuhimiza maendeleo Afrika, ikitarajiwa kuwa itawafanya wahamiaji wabaki makwao. Lakini juhudi za Itali, za kutaka G7 kukubali kupokea wahamiaji zaidi, inaelekea zitapingwa na hasa Marekani.
Michuano ya klabu bingwa Ulaya hatua ya makundi inatarajiwa kuendelea kutimua vumbi usiku wa leo huku michezo minane ikipigwa katika viwanja mbalimbali. Katika michezo ya kundi H Borussia Dortmund watawakaribisha mabingwa watetezi wa kombe la klabu bingwa barani Ulaya Real Madrid katika uwanja wa Signal-Iduna-Park huko Urarumani wakati Apoel Nicosia ikicheza dhidi ya Tottenham. Kundi E – Sevila inacheza na Maribor, Spartak Moscow dhidi ya Liverpool, Kundi F – Manchester city inacheza na Shakhtar Donetsk, Napoli inacheza na Feyenoord na Kundi G- Besiktas inacheza na Rasen Ballsport , Monaco dhidi ya FC Porto.
HUENDA Yanga wakatimiza ahadi yao ya kutangaza ubingwa mapema msimu ujao, hii ni kutokana na usajili wa nguvu wanaoufanya, kwani baada ya kunasa saini ya baadhi ya wachezaji muhimu, sasa wameelekeza nguvu zao nchini Ivory Coast na muda wowote watashusha mtambo wa mabao. Straika huyo, ambaye wanamuwinda kwa udi na uvumba, ni Aristide Bance, ambaye amekipiga katika timu mbalimbali barani Ulaya, ikiwamo Ujerumani pamoja na Afrika. Kwa sasa straika huyo anaichezea timu ya Asec Mimosas ya nchini kwao Ivory Coast, lakini ameshawahi kupita nchini Uturuki akiichezea Samsunspor, pia 1. FSV Mainz 05 ya nchini Ujerumani. Straika huyo ambaye kucheka na nyavu ni jambo la kawaida kwake, pia aliichezea Chipa ya nchini Afrika Kusini katika msimu wa 2015/16, akiifungia jumla ya mabao matatu katika michezo 14 aliyocheza. Kwa ujumla straika huyo mpaka sasa amepitia timu 19, lakini mafanikio yake makubwa aliyapata kwenye soka la Ujerumani pamoja na Ubelgiji, ambapo timu alizozichezea alifunga idadi...
Comments