CCM CHADEMA wajibizana kwa maneno haya

Moja ya habari kubwa za Tanzania leo October 30 2017 ni kujiuzulu kwa Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu ambae pia ametangaza kujiuzulu nafasi zake zote ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM.
Baada ya kauli hiyo AzamTV imemuhoji Katibu Mkuu wa Itikadi na Uenezi CCM Humphrey Polepole ambae amesema “ Ni jambo la kawaida kabisa mtu ambae ameondoka anazo haki zote, wameondoka Wazito kwenye chama hiki na chama kimebaki kimoja kwahiyo huyu sio sehemu ya wazito, ni Mwananchi ambae ana haki ya kufanya hivyo “
Kwenye chama cha Mapinduzi kila kipindi ambacho tumekua tukifanya mageuzi makubwa ambayo yanatoa tafsiri pana ya kifikra na kuonyesha mwelekeo mpya, watu wengi huputika… nina uhakika wako kadhaa ambao wanashindwa kwenda na mwendokasi huu sasa kabla shoka halijawekwa shinani unakimbia mapema ” – Polepole
CHADEMA kwa upande wake kimesema “ Chama cha siasa ni watu na hakuna chama cha siasa ambacho kitasema hatutaki watu, tunampongeza sana kwa uamuzi wake huo na ni uamuzi wa kizalendo, muda muafaka ukifika tutampokea”

Comments

Anonymous said…
How to make money from gambling? - Worktomakemoney.com
How to make money from gambling? · หาเงินออนไลน์ Start with your first bet: kadangpintar · Place a bet on a live horse race · Place a bet in 바카라사이트 an online casino · Step-by-step guide on

Popular posts from this blog

DROO YA KLABU BINGWA ULAYA HII HAPA

Nyumba ya Mbunge Kigoma Mjini Zitto Kabwe yaungua moto

Wanawake wasiowaita waume kwa majina yao India

Cristiano Ronaldo kawaonesha watoto wake mapacha leo

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO

Baada ya Kifo cha Mumewe… Zari Akwaa Aibu 5 #Tazama

hali ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu

Emmanuel Mbasha, aweka wazi haya .