ALICHOSEMA RAIS MAGUFULI BAADA YA KUPOKEA TAARIFA ZA KIFO CHA NDESAMBURO SIASA -


“Kwa masikitiko nimepokea taarifa za kifo cha Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Moshi Mjini, Mzee wangu Philemon Ndesamburo kilichotokea leo tarehe 31 Mei, 2017 katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC iliyopo Moshi Mkoani Kilimanjaro, Namkumbuka Mzee Ndesamburo kwa hekima zake na uongozi wake uliozingatia siasa za kistaarabu”
Hii ni kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa katika salamu zake za rambirambi kwa familia ya Marehemu Philemon Ndesamburo, Viongozi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA ) pamoja na ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na kifo hicho.
Mhe. Rais Magufuli amesema alifanya kazi na Marehemu Philemon Ndesamburo wakati wote wakiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wakati wote walishirikiana, kutaniana na anamkumbuka kwa namna ambavyo alitumia muda wake bungeni kupigania mambo yenye maslai kwa wananchi wa jimbo lake la Moshi Mjini.
Mhe. Dkt. Magufuli ameitaka familia ya Marehemu Philemon Ndesamburo na wote waliguswa na msiba huu kuwa na moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu na amemuombea Marehemu apumzishwe mahali pema peponi, Amina.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

Comments


Popular posts from this blog

wawili wamefariki dunia katika majibizano ya risasi

Jumuiya ya Freemasons imetoa tahadhari nzito kwa Watanzania

Taarifa ya Serikali baada ya kauli za jana za Tundu Lissu

waziri mkuu majaliwa awa mkali

Kilichomkorofisha Mke wa Roma

. Ridhiwani Kikwete amefunguka haya kwa wananchi na baadhi ya viongozi wakae

Spika Ndugai Aagiza Kubenea Kusakwa, Zitto Kufikishwa Kwenye Kamati ya Maadili

Msigwa tunawindwa wabunge wanne CHADEMA -