HAKIMU AJITOA KESI YA MBUNGE GODBLESS LEMA.


Hakimu mmoja anayesikiliza kesi za Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Godbless Lema amejitoa katika kusikiliza kesi ya kiongozi huyo ambapo baadhi zinatarajiwa kuanza kuunguruma Juni 20 mwaka huu baada ya upelelezi kukamilika.
Hakimu amesema kuwa, kiongozi huyo ana jumla ya mshataka manne ya uchochezi ambayo yote yapo mikononi mwake, ndio sababu ameamua kujitoa kusikiliza moja ya mashtaka hayo.
Hayo yalisemwa na Hakimu Mkazi Desderi Kamugisha wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ambapo alifafanua amefikio uamuzi huo baada ya kuona si busara kesi zote hizo kuwa mikononi mwake.
Hakimu Kamugisha amejitoa katika kesi ya jinai namba 441/2016 ambayo Lema anadaiwa kutoa matamshi ya kumkashifu Rais Dkt Magufuli Oktoba 23, mwaka jana wakati wa mkutano wa hadhara viwanja vya Shule ya Sekondari Baraa.
“Kiburi cha Rais akiendelea kujiona yeye ni Mungu, hatafika 2020, Mungu atakuwa amechukua maisha yake. Rais ni mbabe na watu anawaonea, wafanyakazi wa serikali hawana amani, wafanyabiashara hawana amanai.”
Hakimu huyo sasa ataendelea kusikiliza kesi nyingine ya jinai namba 440/2016 ambayo pia inamhusu Lema anayedaiwa kutoa maneno ya uchochezi yenye kuleta tabaka miongoni mwa jamii Oktoba 22, mwaka jana maeneo ya Kambi ya Fisi, Kata ya Ngarenaro wakati wa mkutano wa hadhara.
Kamugisha alisema kuwa ana kesi nne za mbunge huyo ambazo zote zinafanana makosa kasoro siku ya kuyatenda hivyo hakuona busara kuendelea kusikiliza kesi zote wakati kuna mahakimu wengine.
Wakili wa serikali, Alice Mtenga aliieleza mahakama hiyo kuwa upelelezi umekamilika na akaomba Juni 20 maelezo ya wali yasomwe, maombi ambayo yalikubaliwa na mahakama.

Comments


Popular posts from this blog

DROO YA KLABU BINGWA ULAYA HII HAPA

Nyumba ya Mbunge Kigoma Mjini Zitto Kabwe yaungua moto

Wanawake wasiowaita waume kwa majina yao India

Cristiano Ronaldo kawaonesha watoto wake mapacha leo

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO

Baada ya Kifo cha Mumewe… Zari Akwaa Aibu 5 #Tazama

hali ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu

Emmanuel Mbasha, aweka wazi haya .