Mabodi aitaka CCM iendelee kufanya sera za ushindani wa maendeleo 


Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ amesema CCM itaendelea kufanya ushindani wa sera za maendeleo zitakazowanufaisha wananchi wa makundi yote mijini na vijijini.
Kauli hiyo ameitoa leo (Jumamosi) wakati akifungua mafunzo ya Wanawake na Uongozi kwa wanachama na viongozi wa Umoja wa Wanawake (UWT), Mkoa wa Mjini huko Amani Zanzibar.
Dk Mabodi amesema wananchi wa Zanzibar kwa sasa wanachohitaji ni siasa za ushindani wa kisera katika kukuza kipato cha mwananchi mmoja mmoja hadi taifa kwa ujumla.
Amesema taifa lolote linalotamani kuendelea kiuchumi ni lazima wananchi wake wakubali kwa vitendo dhana ya siasa za ustaarabu katika kudumisha amani na utulivu wa nchi ili kufanya kazi za kujiongezea kipato na kukuza uchumi wa nchi.

#mwananchi

Comments


Popular posts from this blog

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO

KENYA :Caroline Odinga akutwa amekufa

mimi nipo sex Lulu diva

mchezaji afariki uwanjani

Mambo 10 ukiyazingatia wewe ni mke bora katika ndoa

Gabo amkana Wema Sepetu

BREAKINGNEWS serikali yamjibu tundulisu