mchezaji afariki uwanjani


Choirul Huda, mwenye miaka 38, alikimbizwa hospitalini siku ya Jumapili lakini muda mfupi baadae ilitangazwa kwamba amefariki dunia.
Katika taarifa iliyotolewa na tovuti ya klabu yake Persela FC , daktari wa timu Yudistiro Andri Nugroho amesema mchezaji huyo alifariki baada ya kupata madhara makubwa kifuani.
Anasema mgongano huo ulisababisha kushindwa kupumua kwa Huda.
Ameongeza kuwa madaktari walijaribu kuokoa maisha yake bila mafanikio.
Mchezo huo uliisha kwa Persela kuifunga Semen Padang 2-0.
Maelfu ya mashabiki wamefika hospitalini alipofia mchezaji huyo aliyecheza michezo 500 ya ligi kuu kwa klabu yake pekee.

 Na BBC

Comments


Popular posts from this blog

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO

KENYA :Caroline Odinga akutwa amekufa

mimi nipo sex Lulu diva

Mambo 10 ukiyazingatia wewe ni mke bora katika ndoa

Gabo amkana Wema Sepetu

Mabodi aitaka CCM iendelee kufanya sera za ushindani wa maendeleo 

BREAKINGNEWS serikali yamjibu tundulisu