RC atangaza kiama wanaoipaka Serikali tope

Makalla ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na wafanyabiashara na wamiliki wa wa hoteli walipokutana kwenye uzinduzi wa hoteli ya kisasa ya Mgwasi Inn iliyopo Mama John Jijini Mbeya.

RC atangaza kiama wanaoipaka Serikali tope
By Godfrey Kahango, Mwananchi
Mbeya. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amewatangazia kiama watu watakaobainika kuipaka tope na kutaka kuichonganisha Serikali na wafanyabiashara kwa kuwakadiria na kuwatoza kiwango cha kodi ambayo ni kinyume na matakwa halisi.
Makalla ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na wafanyabiashara na wamiliki wa wa hoteli walipokutana kwenye uzinduzi wa hoteli ya kisasa ya Mgwasi Inn iliyopo Mama John Jijini Mbeya.
Amesema kuna watu hususani watumishi wasiokuwa wamaaminifu wamekuwa wakiipaka tope Serikali kwa wafanyabiashara na kuleta chuki na kuiona sio rafiki kwa mfanyabiashara kutokana na kuwakadiria kodi isiyoendana na uhalisia wa biashara yenyewe huku akisisitiza kodi ilipwe kwa kiwango halali na si vinginevyo.
“Jamani isionekana mtu kufanya biashara ni adhabu kwa kutwishwa zigo kubwa la kodi. Na wengine wanaipaka tope Serikali ‘eti Serikali hii ni ya hapa kazi tu’ hivyo tumekukadiria kodi hiyo ni lazima ulipe...Hapana hatuendi hivyo na ninaamini tumeshaelekezana watu watalipa kodi kwa mujibu wa sheria na kwa viwango stahiki na si vinginevyo,” amesema Makalla.

Comments


Popular posts from this blog

ILE SINTOFAHAMU YA NANI BINGWA WA VPL HII HAPA

Michezo:Ajibu huyo yanga

ELIZABETH MICHAEL ' LULU' awafungukia wasanii wa bongo move

KUTOKA IKULU:Rais Magufuli amefanya uteuzi mwingine leo julai 6 2017

fahamu kilichojiri nyumbani kwa Tundulisu