Hawa hapa huwenda waka chukuwa nafasi ya Profesa Sospeter Muhongo



Dodoma. Rais John Magufuli, anatarajiwa kufanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri wakati wowote kuanzia sasa ili kujaza nafasi ya waziri wa Nishati na Madini.
Nafasi hiyo iliachwa wazi baada ya Profesa Sospeter Muhongo kung’olewa katika wadhifa huo Mei 24, kutokana na ripoti ya kamati maalumu iliyoundwa na Rais, kuchunguza mchanga wa dhahabu katika makontena 277.
Kamati hiyo iliyoongozwa na Profesa Abdulkarim Mruma ilisema Kampuni ya Acacia, haikutangaza kiasi cha madini yote yaliyokuwa katika makontena 277 ambayo yalizuiwa kusafirishwa nje kwa amri ya Rais.
Matokeo ya kamati hiyo yanaonyesha kuwa thamani ya madini yote yaliyopo kwenye makontena 277 ni kati ya Sh829.4 bilioni na Sh1.439 trilioni, tofauti na thamani iliyotolewa na Acacia ya Sh97.5 bilioni.
Hii ni mara ya pili kwa Profesa Muhongo kung’olewa katika wizara hiyo. Januari 24, 2015 alijiuzulu wadhifa huo baada ya kuhusishwa na kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow ikiwa ni shinikizo la Bunge, baada ya kutolewa kwa maazimio ambayo pamoja na mambo mengine, yalitaka mamlaka ya uteuzi wake imwajibishe.
Vyanzo mbalimbali vimedokeza kuwa Rais Magufuli hana jinsi zaidi ya kufanya mabadiliko madogo ya baraza lake la mawaziri ili kujaza nafasi hiyo huku wanaofaa kumrithi wakitajwa.
Majina yanayotajwa kumrithi Profesa Muhongo, ni pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi na Waziri wa Tamisemi, George Simbachawene.
Simbachawene aliwahi kuhudumu katika wizara hiyo akiwa naibu waziri, kabla ya kuukwaa uwaziri kamili Januari 2015 baada ya kujiuzulu kwa Profesa Muhongo.

Comments


Popular posts from this blog

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAPILI 27.08.2017

Maajabu ya pacha walioungana, wajikuta katika penzi moja .

Picha sita 6 mende wamaajabu duniani

TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMISI 31.08.2017

TANZIA: Aliyewahi kuwa mbunge wa Moshi Mjini, Mzee Philemon Ndesamburo(CHADEMA) aaga dunia

Picha ya Beckham na mtoto wake Serengeti imeleta mjadala hadi kwao

MTWARA:watu watano wanashikiliwa na Jeshi la polisi

MANARA AMKABIDHI JPM KIWANDA

Jux afunguka haya kuhusu vanessa mdee

Marekani yatishia vikwazo kwa yeyote atakaekwamisha uchaguzi DRC