Wanawake wazidi kuikimbia Sudan kusini


Maelfu ya wanawake na watoto kutoka Sudan kusini wamevuka mpaka kuingia nchini Sudan tangu kuanza kwa mwaka huu, wakikimbia ghasia na kitisho cha njaa.
Kwa mujibu wa Shirika la Kuwahudumia Wakimbizi Duniani -UNHCR- Karibu Wasudan kusini laki moja na 37 elfu wameingia nchini Sudan tangu Januari mosi, huku wengine zaidi ya laki moja na 31 elfu wakiwa tayari wamewasili nchini humo tangu mwaka 2016.
Wafanyakazi wa misaada wanaarifu kuwa wengi ya watu hao wanaowasili sasa ni wanawake na watoto.
Mkurugenzi wa Shirika la Msalaba mwekundu, kanda ya Afrika Dokta Faroumata Nafo-Traore wengi wanakuwa wamedhoofika kiafya na wamekuwa na msongo wa mawazo kutokana na hali iliyowatokea huko wanakotoka.
Tangu Desemba mwaka 2013 jumla ya wakimbizi laki nne na 17 elfu wa Sudan Kusini waliingia nchini Sudan. Wengi wao wako katika kambi zilizokuwa Mashariki na Kusini mwa Darfur na magharibi na kusini mwa KordofanxKordofanx
Habari na BBC

Comments


Popular posts from this blog

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAPILI 27.08.2017

Maajabu ya pacha walioungana, wajikuta katika penzi moja .

Picha sita 6 mende wamaajabu duniani

TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMISI 31.08.2017

TANZIA: Aliyewahi kuwa mbunge wa Moshi Mjini, Mzee Philemon Ndesamburo(CHADEMA) aaga dunia

Picha ya Beckham na mtoto wake Serengeti imeleta mjadala hadi kwao

MTWARA:watu watano wanashikiliwa na Jeshi la polisi

MANARA AMKABIDHI JPM KIWANDA

Jux afunguka haya kuhusu vanessa mdee

Marekani yatishia vikwazo kwa yeyote atakaekwamisha uchaguzi DRC