waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu nchemba awajia juu Chenge, Werema

Wanasheria hao wakuu wa serikali wastaafu, ni Andrew Chenge na Jaji Frederick Werema na amewataka wamwache Rais John Magufuli aendelee kulinda rasilimali za umma, zisiliwe na watu wachache
         
Iramba.Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amewachana wanasheria wakuu wa Serikali wastaafu kwa kuwataka waeleze hadharani maslahi walionayo kwenye kampuni za madini zinazosafirisha mchanga nje ya nchi.
Wanasheria hao wakuu wa serikali wastaafu, ni Andrew Chenge na Jaji Frederick Werema na amewataka wamwache Rais John Magufuli aendelee kulinda rasilimali za umma, zisiliwe na watu wachache.
Mwingulu amesema hayo juzi wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na mamia ya wananchi wa Tarafa ya Ndago, jimbo la Iramba.
Alisema Chenge na Werema kwa nyakati tofauti wakiwa wanasheria wakuu wa Serikali, pamoja na majukumu yao mengine, wameshiriki kusaini mikataba mikubwa mikubwa, ikiwemo ya makampuni ya kuchimba madini.
“Kwa akili ya kawaida tu, baadhi ya mikataba mikubwa ikiwemo ya makampuni ya madini, haikuwa sawa… Ndio maana imelalamikiwa kwa muda mrefu,” alifafanua Mwigulu.

Comments


Popular posts from this blog

ILE SINTOFAHAMU YA NANI BINGWA WA VPL HII HAPA

Michezo:Ajibu huyo yanga

ELIZABETH MICHAEL ' LULU' awafungukia wasanii wa bongo move

fahamu kilichojiri nyumbani kwa Tundulisu