IGP Sirro atangaza bingo la milioni 10 Rufiji



Dar es Salaam. Mkuu mpya wa majeshi, IGP Simon Sirro amefanya mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari leo, na kutangaza dau nono la Sh10 milioni kwa atakayetoa taarifa kuhusu mauaji ya Kibiti, Rufiji na Mkuranga.
“Niwaambie ukweli kuwa katika hili, maneno yatakuwa machache lakini vitendo vitakuwa vingi zaidi,” amesema katika mkutano huo.
Pia IGP Sirro amewatangazia kiama madereva wa bodaboda na kuwataka kuacha kuvunja sheria za barabarani kwa makusudi.
“Huu ni wakati wa kutii utawala wa sheria bila shuruti na nimeshaongea na makamanda wa polisi nchi nzima,” amesema
BRIEFING
 Oktoba 2016
Kadhalika, Oktoba mwaka jana aliyekuwa Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho Ally Milandu aliuawa baada ya kuvamiwa na watu wanne, waliompiga risasi mbili.
Novemba, 2016
Novemba mwaka jana, wenyeviti wawili wa vitongoji wa kijiji hicho waliuawa kwa kupigwa risasi.
Januari 2017
Januari mwaka huu, katika kijiji cha Nyambunda, kitongoji cha Mkwandara, watu wasiofahamika walimuua mfanyabiashara, Oswald Mrope kwa kumpiga risasi mbele ya familia yake.
Februari 2017
Tukio jingine ni lile la Februari 3, mwaka huu ambapo majambazi walivamia nyumba ya Mwenyekiti wa kijiji cha Jaribu, Bakari Msanga, ambaye alifanikiwa kuwatoroka.
Hata hivyo majambazi hayo yalipomkosa, yalirejea na kumwaga mafuta, kisha kuichoma moto nyumba yake.
 Februari 24
Februari 24 mwaka huu, majambazi hayo yalimuua ofisa upelelezi, wilaya hiyo, Peter Kubezya na maofisa maliasili wawili

Comments


Popular posts from this blog

ILE SINTOFAHAMU YA NANI BINGWA WA VPL HII HAPA

Michezo:Ajibu huyo yanga

ELIZABETH MICHAEL ' LULU' awafungukia wasanii wa bongo move

KUTOKA IKULU:Rais Magufuli amefanya uteuzi mwingine leo julai 6 2017

fahamu kilichojiri nyumbani kwa Tundulisu