Wanasayansi nchini Marekani wamefanikiwa kupambana na maradhi sugu


Wanasayansi nchini Marekani wamefanikiwa kupambana na maradhi yaliyokuwa sugu kwa dawa za kupambana na vijidudu yaani antibiotics tatizo ambalo lilikuwa tishio dhidi ya sekta ya afya duniani.
Watafiti wameiboresha dawa ya sasa, Vancomycin kwa kutengeneza aina nyingine ya dawa.
Vancomycin ilikuwa ikipoteza uwezo wake wa kupambana na bacteria aitwae enterococci ambaye husabisha madhara kwenye njia ya haja ndogo na vidonda.
Aina mpya ya dawa hii ina nguvu mara elfu moja zaidi na hushambulia vijidudu kwa njia tatu tofauti, kiasi cha vijidudu kushindwa kupambana na dawa hiyo.
Inakadiriwa kuwa vijidudu vilivyokuwa vikipambana na dawa za antibiotics husababisha vifo takriban elfu hamsini kila mwaka nchini Marekani na barani Ulaya.

Comments


Popular posts from this blog

ILE SINTOFAHAMU YA NANI BINGWA WA VPL HII HAPA

Michezo:Ajibu huyo yanga

ELIZABETH MICHAEL ' LULU' awafungukia wasanii wa bongo move

fahamu kilichojiri nyumbani kwa Tundulisu