TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAPILI 27.08.2017
Liverpool wameweka makataa ya hadi Jumatatu, kwa Barcelona wawe wamefikia bei ya Philippe Coutinho, 25. (Onda Cero) Liverpool wanataka kukamilisha usajili wa Alex Oxlade Chamberlain, 24, kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Chelsea pia wanamtaka winga huyo wa Arsenal. (Sunday Mirror) Mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28, imeripotiwa anaitaka klabu yake kumfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika EPL iwapo wanataka asaini mkataba mpya. (Daily Star) Meneja wa Arsenal Arsene Wenger hajakata tamaa ya kumsajili Thomas Lemar wa Monaco, 22, pamoja na Virgil van Dijk, 26, ingawa huenda ikawa msimu ujao. (Sun) Arsenal wanataka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Marco Asensio, 21. (Sunday Express) Paris Saint-Germain wanaendelea na majadiliano ya kumsajili mshambuliaji wa Monaco Kylian Mbappe kwa pauni milioni 166 kabla ya dirisha la usajili kufungwa, ingawa Monaco wenyewe wanataka Mbappe aende Real Madrid. (Sunday Telegraph) Iwapo Kylian Mbappe ataondoka Monac...
Comments