ushahidi madiwani waliojiuzulu kuanika

Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amesema kesho Jumapili ataweka hadharani ushahidi wa tuhuma walizonazo kuhusu madiwani wa chama hicho waliojiuzulu wakisema ni kutokana na kuunga mkono utendaji wa Rais John Magufuli.
Lema na mbunge mwenzake wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari wamewatuhumu madiwani hao wakisema uamuzi wao unatokana na rushwa.
Hata hivyo, madiwani hao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakikanusha tuhuma hizo.
Lema akizungumza na
Mwananchi leo Jumamosi, amesema wataweka hadharani ushahidi huo kesho kabla ya Jumatatu kuupeleka kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

 Na mwananchi

Comments


Popular posts from this blog

wawili wamefariki dunia katika majibizano ya risasi

waziri mkuu majaliwa awa mkali

Kilichomkorofisha Mke wa Roma

Msigwa tunawindwa wabunge wanne CHADEMA -

CHADEMA yafunguka Hospitali aliolaza Tundu Lissu

MTWARA:watu watano wanashikiliwa na Jeshi la polisi

Anaandika Yericko_Nyerere

John Heche kuja na hoja binafsi muda wa Rais upunguzwe