mikutano ya Godbless Lema yazuiwa

Polisi Wilaya ya Arusha imepiga marufuku mikutano ya hadhara ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kwa maelezo kuwa kutakuwa na ujio wa viongozi wa kitaifa jijini hapa.
Pia, kuzuiwa mikutano ya mbunge huyo wa Chadema kunahusishwa na tukio la kuungua moto nyumba za polisi.
Katika barua ya Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP E.Tille kwenda wa Lema  Jumatano, imeeleza mikutano yake imesitishwa.
Mikutano hiyo ilikuwa ifanyike leo Alhamisi na kesho.
Katika barua hiyo, Jeshi la Polisi limeeleza kuwa tarehe ambazo mikutano hiyo, imepangwa zina mwingiliano na ratiba za shughuli za kiserikali za viongozi wa juu wa Serikali inayoishia Oktoba 4.
Pia, amesema janga la moto katika kambi ya polisi lililotokea jana usiku limeleta madhara makubwa hivyo, nguvu kubwa itaelekewa huko.
"Unashauriwa kupanga mikutano yako tarehe yoyote kuanzia Oktoba 5, 2017 pia rejea mazungumzo yangu na wewe ofisini kwangu ya tarehe 29/09/2017," inasomeka barua hiyo.
Hata hivyo, Lema akizungumza na Mwananchi amesema anapinga polisi kuzuia mikutano yake, kwa kuwa ni ukiukwaji wa sheria na haki za mbunge.
Lema amesema sheria ya Bunge kifungu cha nne fasili ya kwanza, kinazungumzia uhuru wa mbunge kufanya mikutano jimboni kwake na kifungu cha 4(1) na (2) vinaelezea uhuru huo wa mbunge kufanya mikutano na pia ni ukiukwaji wa sheria kuzuia mikutano ya mbunge kwenye jimbo lake.
Mbunge huyo amesema anaamini, kuzuiwa mikutano yake ni njama kwa kuwa aawali alipanga kuzungumza na wananchi wa Kata ya Kimandolu ambako diwani wao amejiuzulu na wananchi wa Mjini Kati.
"Kwanza waliniita wakaniambia hali ya kisiasa si nzuri nisiende kufanya mkutano Kimandolu kwa kuwa wananchi wanaweza kuwa na hasira baada ya diwani kujiuzulu, mimi nikawaambia wasiwe na hofu lazima likafanye mkutano," amesema.
Lema amesema anajua polisi wanaamini atazungumzia sakata la kupigwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na pia ziara ya Rais John Magufuli ambayo aliifanya hivi karibuni jijini Arusha.
Amesema anashauriana na wanasheria wake kuona kama akubali barua ya polisi au aendelee na mikutano yake.
Hii ni mara ya pili Lema kuzuiwa kufanya mikutano. Agosti 25 alizuiwa ili kupisha mbio za Mwenge wa Uhuru na mitihani ya darasa la saba na alitii agizo hilo.


  Na mwananchi

Comments


Popular posts from this blog

DROO YA KLABU BINGWA ULAYA HII HAPA

Nyumba ya Mbunge Kigoma Mjini Zitto Kabwe yaungua moto

Cristiano Ronaldo kawaonesha watoto wake mapacha leo

Baada ya Kifo cha Mumewe… Zari Akwaa Aibu 5 #Tazama

hali ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu

Wapiga dili wa madini sasa kukiona

Irine Uwoya: afunguka kuhusu ombi la Dogo Janja kummiliki

hii ndio furaha ya Diamond na zari