DPP akwamisha kesi ya Maxence Melo

Kesi ya kuzuia Polisi kufanya uchunguzi, inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jamii Forum, Maxence Melo (40) na Mwanahisa wa mtandao huo, Mike Mushi, imeshindwa kuendelea baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha ombi la kuifanyia marekebisho hati ya mashtaka.
Kesi hiyo namba 456 ya mwaka 2016, iliyopo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jana ilipaswa kuendelea na ushahidi wa upande wa mashtaka.
Wakili wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi alimweleza Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba anayeisikiliza kesi hiyo kuwa, ilikuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi lakini wanaomba kuifanyia marekebisho hati ya mashtaka chini ya kifungu 234 (1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA).
Hata hivyo, Wakili wa utetezi, Jeremiah Mtobesya alipinga maombi hayo ya kutaka kufanyia marekebisho ya hati hiyo, akidai kuwa tayari mahakama imeshasikiliza shahidi mmoja wa upande wa mashtaka.
“Tunaomba mahakama isikubali upande wa mashtaka kubadilisha hati ya mashtaka kwa sababu hatujaambiwa ina mapungufu gani” alidai Wakili Mtobesya.
Baada ya maelezo hayo, Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 11, itakapoendelea huku akikubali upande wa mashtaka kufanya marekebisho ya hati ya mashtaka.

  Na 

Comments


Popular posts from this blog

DROO YA KLABU BINGWA ULAYA HII HAPA

Nyumba ya Mbunge Kigoma Mjini Zitto Kabwe yaungua moto

Wanawake wasiowaita waume kwa majina yao India

Cristiano Ronaldo kawaonesha watoto wake mapacha leo

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO

Baada ya Kifo cha Mumewe… Zari Akwaa Aibu 5 #Tazama

hali ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu

Emmanuel Mbasha, aweka wazi haya .