Nyumba yamuwekezaji kuvunjwa

Naibu Waziri huyo alitoa, agizo hilo leo alipokuwa ametembelea shamba la mpunga la kilimo cha ushirika Ruvu (CHAURU) ambapo alielezwa kuwa kuna mgogoro kati ya wakulima na mwekezaji wa kichina aitwaye Guo Ming Tang ambaye aliingia mkataba batili na uongozi wa awali wa ushirika huo mwaka 2012 kwa niaba ya CHAURU.
Mwenyekiti wa CHAURU, Sadala Chacha amemweleza Naibu Waziri kuwa mgogoro huo umekuwa wa muda mrefu na kuwa kuziba mfereji huo kumesababisha ekari 24 kutokulimika kwa miaka mitano na kusababisha upotevu wa wastani wa kilo 236,000 za mpunga zenye thamani ya sh. 200,600,000.
Baada ya kuelezwa migogoro kadhaa kati ya wakulima na mwekezaji huyo, ikiwemo huo wa kuziba mfereji na pia kuwauzia maji wakulima,ya kumwagilia kwa saa moja kwa bei ya sh. Laki moja naibu waziri alitoa maagizo kadhaaa sambamba na kuvunjwa kwa nyumba hiyo ya mwekezaji.

 Na eatv

Comments


Popular posts from this blog

sharti la polepole lapata upinzani

wananchi wamshtaki polisi kwakuwanyanyasa

KENYA:Tume Huru ya Uchaguzi yaridhia maombi ya upinzani

Angelina Jolie kuonekana kwenye jarida la ‘Vanity Fair’.

Afisa wa serikali ajinyonga

Viongozi wa G7 waangazia bara la Afrika

UEFA kuendelea kutimuavumbi hii leo

YANGA YASHUSHA STRAIKA WA AFCON

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO