Mara paa Barcelona kucheza Ligi Kuu England EPL

Uwezekano wa Barcelona kucheza Ligi Kuu England utaongezeaka iwapo mchakato wa kudai uhuru Catalan utapitishwa kesho kutwa Jumapili.
Barcelona ikijitoa tu Jimbo la Catalonia, kuhamia Ligi Kuu England
Wizara ya Michezo nchini Hispania imesisitiza kwamba klabu ya Barcelona itapoteza sifa ya kucheza Ligi Kuu ya nchini humo maarufu La Liga iwapo Jimbo la Catalonia litajitenga na kuwa nchi huru.
Uwezekano wa Barcelona kucheza Ligi Kuu England utaongezeaka iwapo mchakato wa kudai uhuru Catalan utapitishwa kesho kutwa Jumapili.
Waziri wa Michezo nchini humo alidokeza kuwa iwapo mabadiliko hayo yatapitishwa jambo hilo litakuwa halikwepeki.
Hata hivyo taarifa zaidi zinasema kwamba Serikali ya Hispania imetangaza kutoruhusu kupigwa kura hiyo ya mabadiliko, huku polisi ikidhibiti masanduku ya kura. Pia Waziri Mkuu wa nchi hiyo amesema kwamba hakuna mchakato wa mabadiliko utakaofanyika nchini humo.
Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amekuwa miongoni mwa watu wanaounga mkono Jimbo la Catalonia kujitenga Hisapania.

Comments


Popular posts from this blog

ILE SINTOFAHAMU YA NANI BINGWA WA VPL HII HAPA

Michezo:Ajibu huyo yanga

ELIZABETH MICHAEL ' LULU' awafungukia wasanii wa bongo move

fahamu kilichojiri nyumbani kwa Tundulisu