Mahakama imetoa siku 14 kwa serikali

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam imetoa siku 14 kuanzia leo mshtakiwa Harbinder Sethi akatibiwe katika Hospitali ya Taifa Muhimbili maradhi yanayomkabili na kinyume cha hapo itamuita Mkuu wa Magereza kumuhoji kuhusiana na hilo.Amri hiyo ya Mahakama imetolewa baada ya Wakili wa serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa kudai kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa leo (Ijumaa) lakini upelelezi haujakamilika na kuomba shauri lipangiwe tarehe nyingine.
Kutokana na hayo kesi imeahirishwa na kusikilizwa tena hadi Oktoba 13, 2017.
Mfanyabiashara Harbinder Sethi anatuhumiwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi pamoja na utakatishaji fedha na kuisababishia serikali kuingia hasara.

 Na eatv

Comments


Popular posts from this blog

ILE SINTOFAHAMU YA NANI BINGWA WA VPL HII HAPA

Michezo:Ajibu huyo yanga

ELIZABETH MICHAEL ' LULU' awafungukia wasanii wa bongo move

fahamu kilichojiri nyumbani kwa Tundulisu