KAMPALA: Katikati ya majonzi, yapata siku 15 tu tangu mumewe, Ivan Ssemwaga ‘Ivan Don’ azikwe huko Nakalilo nchini Uganda baada ya kufariki dunia ghafla, aliyekuwa mkewe, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, anadaiwa kuwatibua Waganda kufuatia kushiriki matukio matano (5) yanayotafsiriwa kuwa ni ya aibu, Amani linayo. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya udaku nchini Uganda, tofauti na ilivyotarajiwa, kama ilivyo kwa baadhi ya tamaduni za Kiafrika, kuwa Zari angekuwa kwenye maombolezo kwa siku arobaini au hadi amalize eda kwa kufi wa na mume huyo, yeye amekuwa akijihusisha na ishu ambazo zinaacha watu midomo wazi. AIBU YA KWANZA Ilielezwa kwamba, siku mbili tu baada ya mazishi ya Ivan, Mei 30, mwaka huu, Zari alitupia video kwenye akaunti yake ya Mtandao wa Kijamii wa Snapchat ikimuonesha mwenye furaha tele huku akikata mauno ya hatari hivyo kushangaza wengi walioamini ni video ya zamani. Ilisemekana kuwa, ili kuonesha video hiyo haikuwa ya zamani, Zari aliambatanisha na maneno ya
Comments